Wednesday, October 24, 2012

Maendeleo ya Nchi "Burundi" Je tunayachukuliaje? Hasasa Kikristo

Picture from Burundi YFC visit www.burundiyfc.org

Ndugu wadau ilifika wakati nachukua kwenye Internet nikiwa natafuta angalao nione maendeleo ya Nchi yetu BURUNDI hasasa kikristo. Ikiwa sisi niwa Kristo nilazima katika hatua zetu za safari twende kama wakristo tusiende kama wa ulimwengu, maana hata biblia inasema yakwamba tumefufuka pamoja na Yesu, lazima tutazamie ya Mbingu na tuache yadunia maana tumekufa kwa dhambi na tamaa zote za ulimwengu; lakini nashangaa sana na wakristo wa leo, ukiwatazama kabisa, hakuna utofauti wa mkristo na mwenye dhambi ao waulimwengu, wote ni sawasawa tu. Na katika maendeleo Dunia nzima, kumejaa maendeleo ya kihuni maana yangu kusema kihuni tunakimbilia ya dunia, yani hakuna maendeleo kikristo ila kuna maendeleo kidunia. 

Mala nyingi hua swala hili napo litekereza linanigusa moyoni, Wenzetu warundi tumelala, nataka kuongelea hasasa warundi tuliopo apa malekani maana tuna fursa nzuri sana ya kuendesha kazi ya Mungu mbele na kukomboa Nchi yetu ya Burundi lakini wengi tumekimbilia ya dunia eti ndipo kuna maendeleo. Unajua tunapo endelesha mbele mambo ya dunia ndo kuleta upungufu wa nguvu za Mungu katika Nchi zetu, na endapo Mungu anatoa mkono wake juu yetu, hayo maendeleo unayo jivunia mwenzangu yatabaki bure, ujuwe yakwamba umesimamiya kiti cha Mungu, endapo anatoa bila shaka utaanguka tena kigafra. 

Mimi kama The Superlative, nisinge penda niitwe jina hilo bila matendo ao kitu cha kuonyesha wenzangu na wadau yakwamba ni jina hilo, na ukumbuke yakwamba mimi the Superlative bila wewe, jina hilo halina uthamani; lakini tukiambatana jina langu na lako likua na uthamani katika jamii yetu. Nilichunguza kabisa ilimladi niangalie yakwamba kuna ma website ya kikristo ila jamani, nijiona aibu kabisa! Si kusema yakwamba ndo kujua ila nilizani labda watu watakua wamegeuka, ila mambo ni yale yale. na ma webisite nimefanikiwa kuona ya kikristo ni haya (ambao yametengenezwa na warundi wako apa USA) www.sfelchoir.com, www.mapambanovijana.com, www.rbfchurch.com, www.cagvoice.webs.com  naya mwisho ni hii blog yangu, www.kaburungunews.blogspot.com; kama kuna zingine website za warundi wako apa USA ambao unajua unaweza niambia labdazipo, ila kwa binafsi nimefanikiwa kupata hizo. Mengineo mengi ya dunia, tuseme ya kisani, na ukiangalia ndo yanajulikana kushinda yetu sisi wakristo. hilo jambo linaniumiza sana, wakristo naomba tuwe na umoja tuwaonyeshe wadunia yakwamba uzima tele na raha vimo ndani ya Yesu, tuungane mkono tuonyeshe Vijana wenzetu yakwamba Uzima ndani ya Yesu ni raha tupu. Lakini chuki na upuuzi ndo vina tawala kati yetu sisi nawakati tuna jiita niwakristo. 

Na katika swala hilo, madau na mashabiki wangu wengi ni watanzania na wa congomani ndo maana natumia kiswahili katika blog yangu hii, hili jambo linaniumiza sana, ni aibu kua ma mashaniki wengi wa Nchi za Nje nawakati wapo wengi Nchini kwenu ila hakuna hata mmoja wa kusaidiana. Sasa warundi, tukitazama safari yetu kabisa, twaelekea wapi? maana hata wao watanzania nimekuta wanazo blog nyingi sana zinazo shiriki ukristo, na hata katika Nchini kwao wana ma radio mengi sana ya Kikristo , lakini sijawahi kusikia ivo katika Nchini kwetu, kama zipo tafadhari nitumie link hizo, utakua umenifurahisha na utakua umesaidia wengi ambao hakufahamu ivo.  

Ombi langu nikwamba: kama yeyote yule mrundi, haijalishi unaishi Nchi gani, kama una uryuzi  wa kutengeneza ma website ao blog, tafadhari kama wewe ni mkristo tengeneza blog ao website ya kikristo na tuindeshe Injili ya Yesu Mbele, wengi wataokoka wengi watamurudilia bwana kutokana na Uryuzi wako. Kama huna fursa hiyo ao unaitaji kua jinsi ya kutengeneza, na kukaribisha uongee nami kupitia contacts zangu tutaelekezana. napenda pia kuahisi tutembelee webiste hii www.burundifyc.org kama unazo support tafadhari support Nchi Yetu iendelee mbele. 


Burundi FYC www.burundifyc.org "You can change lives today by Christianity


Amani ya Bwana awe nanyi siku zote
The Superlative Kaburungu