Wednesday, November 28, 2012

Kama kawaida yangu, Afro Shemeza niko naipamba moto!

VIZIO Computer -One In all-

Ndugu wadau kama nilivyo sema yakwamba naenda kuanza kununua vifaa vipya, kama hii Computer mpya nimenunua. Wengi hua wananunua Mack, Apple Computers, ila mimi najaribu kuwa mttu wa aina yake mwenyewe (Unique). Hii Computer kweri ni ya aina yake, na kuhusu uhariri wa video kweri nimeipima ina nguvu na program yote ile nataka naweza tuitia tena siku si nyingi nitawapa nyimbo ninazo zitengeneza. Mukiendelea kutembelea www.burundiangospel.com mutakua munaona video za waimbaji wengi mbalimbali ambazo Afro Shemeza imetengeneza. Nataka kuaeleza yakwamba kaka yangu "Manirakiza Silas" yeye amechagua kuisimamia Afro Shemeza, kama vile munajua kwasasa nina makampuni ma 3 (Afro Shemeza Studios/Stores, Burundian Gospel Entertainment, Quality Life Solution, Inc.) QLS, Inc ndo inaongoza ao itakae ongoza kila kampuni yote ile itakao kuja nyuma, bado sijaianzisha vizuri kazi na matumizi ila siku si nyingi nitaweka wazi kazi ya kampuni hiyo. 

Apa ni ofsini mwangu. Iyo Kubwa ni ile VIZIO Computer mpya, na kama munavyo ona ninazo laptop mbili "HP Laptop & Mack Book Laptop" Kazi si mchezo! Ivyo vyote navitumia kuhakikisha uhariri wa video unakwenda sawa. Mda karibuni naenda kununua vifaa vingine. Napenda nipe Shukrani kaka yangu na mkewe "Silas & Zabibu" kwa usaidizi wao wanao fanya kabisa mkubwa ili waweze kununua vifaa hivi! 

Endeleeni kunitembelea nitakua nawaonyesha vifaa vipya. Karibu kwa kampuni yenu ambao mna amini "Afro Shemeza Studios" 

Wednesday, November 21, 2012

Shukrani kwa wale wote munayo saidia kazi zangu, Mungu awabaliki

Nataka nitowe Shukrani kwa wale wote wanao nisaidia katika kazi zangu. Nashukuru mkurugenzi wa SYUB SHOW ambao inawaburudisha habari za warundi hapa marekani na Nchi mbalimbali. katika video hiyo matangazo yangu utayaona kuanzia kwenye 5:55 

Nawashukuru na wale woooote munao tangaza kazi zangu, mukiamini yakwamba kazi zangu zina faida katika Jamii. Najua ni mupo wengi munao niombea ili niendelee mbele, nisisahau kuwa shukuru wa dau wangu wa karibu ambao munapigia simu mala kwa mala ili mujue kazi zangu zinaendeleaje, Hasasa na wale ambao mumetoa mchango ikiwa pesa ao mchango wote ule wa kuinua kazi zangu. Nawapenda sana nyote, nina imani yakwamba mutaendelea kua mashabiki, wadau hata na marafiki wa karibu sana. Maombi muhimu katika kazi kama hizi, pasipo mkono wa Mungu hatutoweza kufika pale pote. Ila kwa mkono wake, tutaweza. 

Natarajia kufanya Kolabu CD na waimbaji warundi wa nyimbo za Injili kutoka USA, kolabo hiyo ni tofauti na kolabo zingine, ila mutaona tu. Mambo ya kikamilika mutajua. musisahau kuitembelea www.burundiangospel.com maana ni moja wapo wa kazi zangu, sasa wadau mukiitembelea muna niinua kama kawaida. 

Amani ya BWANA awe nanyi 
The Superlative Kaburungu 

Thursday, November 1, 2012

Burundian Gospel kuanza kazi rasmi, Fursa mpya ya mziki wa Mungu kwa warundi

Nimeanzisha Kampuni Mpya "BURUNDIAN GOSPEL". Kwa siku nyingi nikiwa naongea na wadau wangu, hua wanadai yakwamba hakuna Entertainment katika kazi ya Mungu. Hasasa nikiwa naongea nawale wanaojifasha ni wasanii ambao wanaimba nyimbo za mapenzi hua nawashauri ili tuweze kumutumikia Mungu ila wakadai yakwamba katika nyimbo za Injili hakuna Entertainment. Basi ndugu wadau nimeanzisha rasmi Kampuni ya BURUNDIAN GOSPEL Entertainment ambao itatangaza nyimbo ya Injili na kusambaza kazi za waimbaji. Unapewa karibu kama wewe ni mrundi ambao unaimba nyimbo za Injili na unataka kazi zako zisambazwe na kuuzishwa. 

BURUNDIAN GOSPEL inasaidia watu ambao wanamuimbia Mungu (nyimbo za Injili), kama wewe ni muimbaji tofauti na Injili basi BurundianGospel haipo tayari kukusaidia kwa lolote na  samahani sikwamba tunauchaguzi ao upendeleo ila maono yetu nikwamba kazi ya Mungu isonge mbele. 

Na kwa hivyo sasa naenda kuanza kazi na studio yangu Afro Shemeza Studios (Audio & Video Productions), niko najiandaa kununua vifaa vipya na siku si nyingi nitawaonyesha vifaa na mengi mutakua munayajua kwa site hii ya www.burundiangospel.com". Siku si nyingi nitawajulisha nyiye nyote ambao muna ma band ao choirs, Videos na Audio zenye aina yake zinakaribia kuwafikia, itakua ni bahati yako kuitumia kampuni yangu ya Afro Shemeza Studio. 

Nataka nitoe shukrani zangu kubwa kwa Emmanuel Irankunda AKA "Lil Ace". Kijana huu amenifsaidia sana katika utengenezaji wa burundiangospel.com site. Kwa uhariri na utengenezaji wa hari ya juu kuhusu website yako nakusihi umupe na fasi kijana huu akutengenezee maana yuko juu. Na katika jamii yetu (Burundian Community) ya kisasa kwa warundi tunaitaji watu kama hawa ambao wako tayari kutusaidia katika mambo ambao hatuko tayari kukamirisha. Usikae nyumbani Kijana yote yule, nenda shure ao tumia kipaji chako ili mambo ukaweze kua kitu muhimu katika maisha yako na jamii. Mungu ambaliki Kijana huu, na tafadhari shirikiana nami kwa maombi kwa kumushukuru kijana huu na kumuombea balaka katika maisha yake. 

Nndugu wadau hizi nina kampuni tatu zinaenda kutumia kwa pamoja yani kama kolabo: "BURUNDIAN GOSPEL", "Afro Shemeza Studios/Stores" na hizo zote zifunikwa na kampuni yangu kubwa sana ambao natarajia kuingiza katika jamii yetu, nayo ni hii "The QLS, Inc. -Quality Life Solution-. Kwa siku chache nitawajulisha habari nyingi kuhusu Kampuni hii, na hakuna kampuni nyingine ambao nafikiri nitafanya maana izo tatu zinatosha, nataka kwanza niziinue. CAG Voice Entertainment imefinikwa na BurundianGospel Entertainment; msije mukashangae kwanini siitumii tena. 

Basi nawaalika ngudu zangu kua mnatembela www.burundiangospel.com mala kwa mala kwasababu tutakua tuna post mambo mapya kila kukichapo. Tembelea na uwaalike ngudu zako ili kazi ya Mungu iendelee mbele! 

Amani ya Bwana awe na nanyi!
The Superlative Kaburungu