Monday, October 15, 2012

Maandalizi ya Mpinga Kristo........., Umoja wa Dini 5O wazua Balaa! Papa Benedict, Lutheran wahusika,Makanisa Mengine yajiweka kando pia Quran na Biblia zasomwa kwa p

Papa Benedict 
  • Wakristo tuwe macho, maana tunaukaribia wakati mgumu, Papa Benedict anaandaa upingaji mukubwa kwa wafuataji wa Jina la Yesu, hakikisheni mumeyashika ya Bwana Yesu aliyo yasema! 


Wakati wengine wakiendelea kubishania uhalali wa ibada za mafuta na vitambaa, hatua kubwa ya kufikia umoja wa kidini yaani United Religious, utakaokuwa na nguvu kuzidi Umoja wa Mataifa (UN) imefikiwa hivi karibu, baada ya dini zaidi 50 kuandaa ibada siku ya Jumapili na kutumia Bibilia na Qura’n.

Taarifa iliyonukuliwa na Gazeti la New York Times, ilisema: “Mihimili mikuu mitatu kuelekea mfumo mpya wa dunia ambayo ni Umoja wa kiuchumi duniani, Serikali moja na Dini moja. Masikio ya wengi yameelemea kwenye mihimili miwili zaidi kuliko ule wa tatu ambao wameupuuzia. Lakini huu wa tatu ambao ni dini ya pamoja (kwa maana ya imani moja) ndio usukani na sasa unakaribia kufikiwa. Huu ndio unaojulikana kama ‘Interfaith.’ 


Makongamano na mikutano inaendelea kuongezeka kwa kasi siku hadi siku duniani, huku viongozi wakuu akisisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja. Imani ya kuwa na dini moja"Interfaithimekuwa ikisisitizwa kote duniani na viongozi wa dini mbalimbali wakitumia mashirika (NGOs), mashirika ya misaada, na taasisi mbalimbali, wanasisasa wakubwa wametumiwa kuipa msukumo kwa fedha nyingi katika sayari hii.”
Kisha taarifa hiyo iliongeza: “Hivi karibuni baadhi ya makanisa katika Amerika yamekwenda mbali zaidi katika suala hilo. Juni 26, mwaka huu, Kathedral ya Kitaifa (National Cathedral) katika Jiji la Washington D.C. iliandaa ibada ya pamoja  na zaidi ya makanisa 50 yalishiriki kusoma Quran wakati wa Ibada ya Jumapili.”
Wachambuzi wa siasa dini wanaeleza kuwa hiyo ni hatua katika mkakati mkubwa wa kuundwa kwa shirikisho kubwa la kidini katika kipindi cha mpito kuelekea kuzaliwa rasmi kwa umoja wa kidini  ulimwenguni, ukishinikizwa kwa kipengele cha haki za Binadamu.
Somo kuu katika Jumapili hiyo lilikuwa “Kushirikishana imani, Kushirikiana maombi na kuelewana.” Lengo likielezwa kuwa ni kuonesha upendo wa Wakristo kwa Waislamu waishio Amerika.
Miongoni mwa makanisa yaliyoshiriki ni: Christ Church lililopo jijini New York City,
All Saints Church lililopo Pasadena California, Park Hill Congregational huko Denver,

Hillview United Methodist lililopo Boise, Idaho First United Lutheran, katika mji wa San Francisco, St. Elizabeth's Episcopal Church, huko Honolulu, Makanisa makubwa (dini mbalimbali) yapatayo 26 katika Amerika yamehusika na mpango huo. 

Interfaith Logo 


Imeelezwa kuwa usomaji huo wa Quran ni mpango maalumu wa kulainisha dini zenye misimamo mikali ili kuonesha kuwa upo uwezekano wa kufanya ibada pamoja na kumaliza tofauti zilizowatenga zamani.
Mpango huo mkubwa unatarajiwa kua endelevu ukijumuisha Wakristo, Wayahudi na Waislamu kwa njia ya kusikia na kusoma aya kadhaa, za Qur'an mara kwa mara ili watu wazoee kuwa pamoja na mwisho waunganishe mioyo yao pamoja na kuabbudu pamoja.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mpango huo, Interfaith, Waamerika wana uhuru wa kusoma Quran popote wanapotaka. Lakini kwa Wakristo hawana nafasi ya kusoma na kujifunza kitabu hicho, hivyo kuwepo kwa utaratibu wa kuisoma kila Jumapili wanapokutana kanisani kwenye Ibada na kutawafanya waielewe na kuwa na ‘umoja’ na Waislamu na kuonyesha kutowabagua; jambo ambalo linaonesha dalili ya kuzaliwa kwa kitu kipya duniani.
Wakati huo huo, baadhi ya viongozi wa Kikristo duniani hawako radhi na muendelezo huo. Brannon Howse, mmoja wa viongozi mashuhuri alisema: “Watu hao wamekana uungu wa Yesu Kristo; wamekana ukweli wa maandiko matakatifu; wamekana uvuvio wa Biblia, ni vipi tushirikiane nao na kusoma kitabu chao kwenye ibada zetu?” 


Kisha aliendelea: “Inasikitisha, hii siyo mara ya kwanza. Ukweli ni kwamba umoja huo umepata nguvu miongo kadhaa na baadhi ya wakuu wa dini ulimwenguni wamehusika.
Kwa mfano; habari zilizopatikana kupitia CNS zinaeleza kuhusu muungano mkubwa ‘interfaith’ wakati Papa alipotembelea jiji la Washington 2008.”
Alisema kuwa wakati Papa Benedict XVI alipofika kituo cha, Pope John Paul II Cultural Center kilichopo Washington kwa mkutano wa jioni wa dini zote ‘interfaith’ zilikuwepo dini mbalimbali ambazo hapo awali isingekuwa rahisi kukutana na kuabudu pamoja. Waislamu, Wahindu, Wayahudi na dini nyingine zilipata nafasi zilishiriki; isipokuwa Assemblies of God,hii haikuthubutu hata kusogelea.
Viongozi wa Dini kubwa katika Amerika wanahusika sana na umoja huo "Interfaith movement," kwa mfano; Brian McLaren, mmoja wa viongozi wa juu wanaoendesha umoja huo, inasemekana kuwa mwaka 2009 alisherehekea Ramadhan na hata kuvaa mavazi yanayovaliwa na wahusika.
Katika sherehe hiyo; Rick Warren, mshirika wa Baraza la Uhusiano wa Nje, alikuwa Mgeni rasmi na mnenaji kwenye Kongamano la kitaifa la Waislamu huko Amerika ya Kaskazini, (Islamic Society of North America).
Baadhi ya viongozi wa makanisa wakiwemo Rick Warren, Robert Schuller, Brian McLaren, Richard Cizik na Bill Hybels walitia sahihi barua kwa Jumuiya ya Kiislamu iliyokuwa na kichwa kisemacho;  ‘Kumpenda Mungu na jirani yako’
Barua hiyo iliweka bayana kuwa viongozi wa Kikristo wanamtambua Allah kuwa sawa na Mungu wa Wakristo.
Barua hiyo ilisema:“Kabla hatujashikana mikono; katika kukubaliana na barua yetu, tuwatake radhi kwa kuomba msamaha kwa Muumba wa wote. Kwa Waislamu muumbaji ni Allah.
Kwa barua hii, baadhi ya viongozi wa Kikristo wanamuomba na wanatubu kwa jina la Allah, na wanamtambua kuwa ndiye Mungu.”
Kama tulishindwa kurejesha amani na kuwa pamoja, sasa tumesahihisha mawazo yetu na kwamba tunaweza sasa kutakasa nafsi zetu.”
Barua hiyo ndiyo iliyozua hofu duniani kuwa  huenda wakati sasa umewadia wa baadhi ya viongozi kudhihirisha hali ya vuguvugu  na kukosa msimamo wa kiimani.
“Kwa kweli  huu ni usaliti wa hali ya juu, kuandika barua na kueleza kuwa Allah ndiyo Mungu anayeabudiwa na Wakristo  ni mwanzo wa kuelekea katika  dini moja na utawala wa Mpinga Kristo,” alisema Mchungaji Jonathan Emmanuel, wa Nigeria.
Alisema kuwa anautazama mwelekeo huo kama jambo la hatari kwa kuwa Biblia katika  kitabu cha
Yohana 14:6 , Yesu anasema: “...Mimi ndimi njia, na kweli na uzima; mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.”
Kiongozi huyo alisema kuwa ukweli wa ki-Biblia uko wazi na wala hauna kificho kuwa Yesu ndiye njia pekee ya kufika mbinguni. Ikiwa unaamini hivyo  ni vipi uandike tena barua ya hatari kama hii ya  kumhusisha Allah na ufalme wa Mungu?
Kisha aliongeza: “Katika amri kumi; awali kabisa tunakutana na maandiko yasemayo; “Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usifanya sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni , wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao, nami nawarehemu maelfu  wanipendao, na kuzishika amri zangu.”
 (Kutoka 20:3-6) 

BAADA YA WAISLAMU KUCHOMA MOTO MAKANISA TAREHE 12 MWEZI HUU.HILI NDILO TAMKO LA ASKOFU MKUU WA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD, DK. BARNABAS MTOKAMBALI.

Oktoba 12 mwaka huu, matukio mabaya na yenye kutia doa sifa ya amani umoja na Utengemano wa Taifa la Tanzania, yalijitokeza huko Mbagala Jijini Dar es Salaam, wakati watu wenye jazba wanaoaminika kuwa ni Waislamu wenye msimamo mkali walipovamia makanisa saba ...na kuyachoma moto eti kwa kulipiza kisasi cha mtoto aliyekojolea kuran katika utani wa kitoto.
Katika mkasa huo ambao ni kama muendelezo wa ghasia zingine zilizotokea kule Zanzibar miezi michache iliyopita na kuteketeza makanisa mbalimbali mbali na kuharibu mali za kanisa na zile za watu binafsi.
Tukio la Mbagala limesababisha makanisa saba kuharibiwa vibaya, mali kuibiwa na hata kuhatarisha maisha ya watanzania na kuwafanya waishi kwa hofu na kupoteza matumaini.
CHANZO CHA TUKIOKwa mujibu wa walioshuhudia, Polisi na wahusika (Waislamu) chanzo cha ghasia hizo na mabishano ya kitoto baina ya watoto wa dini ya Kiislamu na kikristo, waliobishana kuwa ikiwa mtu atakojolea kuran na kuitemea mate atageuka mbuzi au nyoka.
Lakini baada ya tukio hilo la kitoto watu walilikuza na kulipeleka kwenye misikiti na hivyo kuchocheza ghasia. Kimsingi tukio lenyewe ni jepesi sana ukilinganisha na matokeo yake. Ukweli kwamba waliofanya utani huo ni watoto na chanzo chake ni mabishano ya kitoto, unatia shaka kuwa huenda kuna hoja nyuma ya pazia ambayo isipotazamwa kwa makini inaweza kulete matokeo mabaya sana.
Jambo linalonitia shaka ni kufanana kwa matukio ya kuchomwa moto kwa makanisa ya Zanziabar na ya Mbagala ambapo hakukuwa na uhusiano wa vyanzo vya ghasia na makanisa husika.
Mfano; Ghasia za Zanzibar zilizopelekea kuangamizwa kwa makanisa zinaelezwa kuwa zilitokana na kikundi cha Kiislamu cha Uamsho wa Mihadhara, kilichokuwa kikiandamana kudai mjadala wa Muungano, lakini zikaishia kwenye uchomaji wa makanisa, hapa hauonekani uhusiano wa kanisa na Muungano; nalazimika kujiuliza kulikoni?
Vivyo hivyo tukio la Mbagala halina uhusiano wa moja kwa moja na kanisa kwa kuwa hakuna ushahidi wala hata tetesi kuwa mtoto huyo alitumwa na kanisa lolote. Wahusika wa dini ya Kiislamu akiwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, analielezea tukio la kitoto kama lisilostahili hata mtu kufunguliwa mashtaka bali kuelekezwa tu. Ni vipi lisababishe uchomaji wa makanisa?
MAKANISA YALIYOCHOMWA MOTOKatika ghasia hizo za aina yake, makanisa saba yamethibitishwa kuharibiwa kwa kuchomwa moto, kupasuliwa vioo, viti na kuibiwa vyombo vya muziki na jenereta. Makanisa hayo ni TAG Kizuiani, Agape, Kibonde maji, SDA Sabato, Mbagala Kizuiani, Katoliki Kristo Mfalme Mbagala Rangi Tatu, Anglican Mbagala Kizuiani, KKKT, Mbagala Zakhem na TAG, Shimo la Mchanga.
Pamoja na majengo hayo kubomolewa kwa viwango tofauti mengine yakichomwa moto, pia wahusika waliiba Genereta, na vyombo vya muziki vya makanisa hayo na kuvunja magari na baadhi yao kuchomwa moto.
Choko choko zilizinazoweza kuwa cahanzo cha matukio hayo ni:
Januari sita mwaka huu, kikundi kimoja kinachoitwa JUAKITA, kiliitisha kongamano la kujadili katiba mpya Tanzania, kwa upande wa Waislamu. Katika kongamano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kulitolewas kauli za kichozi kama:
1. Lazima Rais ajaye atoke Zanzibar
2. Kukabiliana na ukuaji wa kasi wa dini ya Kikristo
3. Kupinga Muungano ili kuupa nguvu Uislamu
4. Kupigana kufa na kupona kutetea maslahi yao wakati huu wa kuandaa katiba mpya.
Kauli hizo zilitolewa na Sheikh Nasoro Mohamed, kutoka Zanzibar, ambaye alikuwa mgeni rasmi. Baadaye zikaandaliwa kanda za CD zilizosambaza ujumbe huo.
Uchunguzi unaonesha kuwa uchochezi huu umekuwa ukiwaandaa watu kusubiri vijitukio vidogo tu ili kulipua ghasi. Tuliona jinsi makanisa yalivyochomwa kule Zanzibar. kwa kuwakumbusha tu makanisan yaliyoangamizwa katika tukio hilo ni: EAGT, Elimu Pentecost na TAG, Anglikana, Katoliki na FPCT.
Ni jambo la kusikitisha kuwa matukio haya yanatokea siku mbili tu kabla ya maadhimisho ya miaka 13, ya kifo cha Rais wa Kwanza, Mwl. Julius kambarege Nyerere. Leo hotuba na midahalo inarindima kila mahali kumuenzi Nyerere, lakini wengi wetu tukiwa tumejaa majozi baada ya nyumba zetu za ibada kuharibiwa katika matukio yanayoashiri hatari kubwa.
Hofu yangu ni kuwa, roho hii ya ubaguzi wa kidini ambayo Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliifananisha na dhambi ya kula nyama ya mtu, imekuwa ikiyatafuna mataifa ya Afrika kama ifuatavyo:
1. Mwaka 2000, vuguvugu la kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu (Sharia), lilianza kwenye majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria, miaka michache baadaye majimbo kadhaa yakajitangazia sheria hizo na tangu wakati huo kumekuwa na mapambano yasiyoisha. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni zaidi ya Wakristo 500 wameuawa kikatili na makanisa kuchomwa moto.
2. Roho hii imekuwa ikienea kwa kasi katika maeneo mbali mbali ya Afrika ambapo imelikumba taifa la Mali, majimbo ya kaskazini tayari yametangaza kujitenga na kuna vuguvugu lenye kuhusisha mapigano ya silaha.
3. Itakumbukwa kuwa miezi michache tu ilizopita vuguvugu hili la kudai utawala wa kidini liliibuka nchini Kenya ambapo watu wanaojiita wanaharakati walianzisha madai ya kutaka eneo la Pwani kujitenga na Jamhuri ya Kenya na kujitangazia taifa la Kiislamu.
4. Katika tukio hilo inasemekana mtoto huyo alitengenezewa mabishano ya kitoto kuwa akichoma kurani atakuwa chizi naye akabisha
kisha akapewa kiberiti na kurani akachoma tena walioandaa
mzaha huo wakamkamata na kumpeleka mahakamani.
Tukio linalofanana na hilo lilitokea tena Bagamoyo mkoani Pwani
ambapo mtoto wa kike alishtakiwa na hata kuhukumiwa kifungo
kwa madai ya kuchoma kuran lakini tukio lilikuwa katika mabishano
ya midhaha ya kitoto
WITO WANGUNatoa wito kwa Wakristo wote nchini kujiepusha na mizaha
inayoweza kutengeneza sababu za kulipuka kwa ghasi na kutengeneza
mwanya wa watu wenye nia mbaya kutekeleza agenda zao zaria Ili
kulinda amani umoja na utengemano wetu, nawasihi viongozi wa makanisa
kuonya na kukemea waumini na watoto wetu wasishiriki kwa namna yoyote ile mizaha inayopelekea kuchoma au kuharibu vitabu au nyaraka
za kidini.
Nawasihi watanzania wote kwa ujula kujiepusha na mizaha ya kidini inayoweza kuchafua amani yetu, na pale jambo lolote lenye kukera linapotokea tujiepushe kuwa mawakala wa shetani wa kueneza chuki badala ya amani na upendo.
USHAURI WANGU KWA SERIKALI NA VIONGOZI Nawashauri viongozi wa Serikali ambao leo wanatoa matamko na kushiriki midahalo ya kumuenzi Mwl. Nyerere kukumbuka kuwa huyo alikuwa na mapenzi makubwa na amani na umoja wa taifa. Kwa hiyo kumuenzi kwa vitendo ni kudumisha utawala bora, unaofuata sheria usio na chembe ya ubaguzi wa aina yoyote.
Kulipuka majukwaani kumuenzi Nyerere bila kuilinda na kuitetea amani ya nchi ni kujidanganya.
Ni wajibu wa kila Mtanzania kutii sheria na mamlaka kwa kuwa zimewekwa/kuruhusiwa na Mungu, hivyo kuziasi ni Kumuasi Mungu, yaani ni dhambi. Hivyo kila Mtanzania anastahili kukumbuka wajibu wake wa kutii mamlaka.
Viongozi wenzangu wa dini wakumbuke kuwa wana wajibu mkubwa katika jamii, na jamii inawasikiliza hivyo ni vyema wakawa makini katika matamshi na maelekezo yao ili wasiwe chanzo cha kuchochea vurugu za kidini na uvunjaji wa amani.
Pia ningependa kuwashauri viongozi wa serikali kusimama imara katika kusimamia sheria na haki, na kuepuka kauli au vitendo vitakavyofanya baadhi ya watanzania kudhani kuwa hawatendewi haki.
Ni vema ieleweke kuwa matukio kama haya ya uvunjaji wa amani yasipodhibitiwa na kukomeshwa haraka yanaweza kuumba chuki ambayo inaweza kuibua mlipuko mkubwa na machungu kwa wananchi na matokeo yake yakawa mabaya kwa Taifa zima. Hekima na busara inatufundisha kuwa tusipoziba ufa tutajenga ukuta.
Ni vyema wenye dhamana ya kuongoza wakakumbuka kuwa wanawajibu mbele ya Mungu aliyewaweka au kuwaruhusu kuingia madarakani na siku moja watatoa hesabu mbele zake.
Ni vyema viongozi wa Serikali wakajizuia kufanya maamuzi yanayoashiria upendeleo kwa baadhi ya makundi ya kidini na kukiuka utawala wa sheria, mfano; kutii waandamanaji na kuwaachia bila mashrti watu waliokamatwa kwa mujibu wa sheria kuna jenga kiburi kwa makundi yenye kiu ya matumizi ya nguvu na kujenga hofu kwa pande zingine.
Ni vyema mamlaka zikasiamama katika sheria na kufanya hukumu kulingana sheria badala ya kuamua mambo ya kisheria kisiasa.
WITO MAALUMU KWA VIONGOZI WA DININitumie nafasi hii kuwasihi vingozi wenzangu wa dini, kusimama imara katika kuombea taifa na kuhubiri kwa nguvu ili kukabiliana na giza la kiroho ambalo linatishia kuifunika nchi.
Takwimu za karibuni kabisa za utafiti uliofanywa na taasisi ya Washnton DC iitwayo, Pew Research Centre, na kurushwa na Televisheni ya CNN, Katika kipindi chake cha Inside Africa, zilionesha kuwa watanzania asilimia 93, wanaamini mambo ya ushirikina na uchawi wakati Uganda ni asilimia 29 na Kenya ni asilimia 27. Tu. Mahali ambapo giza la kiroho limezingira kiasi hiki ni lazima matukio ya kishetani yashamiri tuchukue hatua.
Mwisho, natoa wito kwa watanzania wenzangu tuulinde umoja, amani na utengamano wa taifa letu, tusikimbilie dhambi ya ubaguzi kwa kuwa tukiiruhusu itatuangamiza sote. Tuliombee taifa letu na kukiwa na mbegu ya chuki tuimalize kwa njia ya majadiliano na vikao vya pamoja vinavyohusisha viongozi wa dini zote na serikali pia.



Imetolewa leo 14/10/2012
Na Dk. Barnabas Mtokambali
Askofu Mkuu wa TAG

Jikaze uyashinde mapito

Mapito unayo pitia ndugu yangu ni mda

Ndugu zangu wapendwa, na wasalimu katika Jina la Yesu. Wadau wangu wote na washiliki wa blog yangu hii, leo ningependa tukumbushane machache kuhusu neno la Mungu, safari turio nayo ni ndefu sana, tena tukumbuke ya kwamba safari haikosi makwazo. 

Kitabu cha Jeremiah (YEREMIA) 29:11 panasema: "Maana ninajua mawazo niyowawazia, asema BWANA, ni mawazo ya Amani, wala si ya mabaya; kuwapa ninyi Tumaini siku zenu za mwisho (kwa bibilia ya kingereza siku za mwisho ni: Future "siku sizajo mbele"). Hata kama unapitia hayo, ikiwa ni shida, magonjwa, mateso, majaribu, mikosi, nuksi, etc, Ujue kwamba Mungu anakuwazia mema. Hayo yalio kupata si lengo la Mungu, ndo maana anakuandalia mpango mzuri wa kukutoa katika mapito hayo. Bwana yesu alisema katika kitabu cha YOHANA 14:1-3 "Msifadhaike miyoyoni mwenu, mumwamini Mungu muniamini na Mimi. Nyumbani kwa Baba kuna makao (mazuri) mengi, kama hazingekuwepo ninge waambia, tena naenda kuwaandalia pa kwenu. Kwa maana naenda kuwaandalia pa kwenu, nitakuja kuachukua, ili nilipo na nyi muwepo."Alipo Yesu hakuna Shida, magonjwa, matatizo wala majaribu, etc. ila kuna furaha na Amani tele. Basi alipo Yesu lazima na wewe uwepo, ndo ahadi yake njema alio agana nasi.  Tukumbuke nabii Musa, Mfalme Farao alifanya amri ya kuuwa watoto wakiume ila Bwana akapanga mpango wa kumuokowa. Mpango wa Farao (hesabu kama Shetani ao aduwi) hukumufikia Musa. Kuna mpango wa Mungu wa kukuokoa ambao bado hujafichua, subiri kwa Imani utaona Mijuiza. Hatuwezi kujua mawazo wala mpango wa Mungu, ila tunalo tumaini katika maandiko yale ya YEREMIA 29:11. Mawazo yake kwako ni ya Amani; ni kwamba anakuwazia mema na anakutakia Amani katika shida zako. Tukifikiria kuhusu hari ya hewa, kuna Summer, Spring na Fall; mda wa fall hua kuna balidi kubwa sana na kuna Nchi ambazo zinafikiwa na balidi kali kabisa hadi mtu kufikiri ahame. Lakini huwezi kutosha matumaini kwasababu ya balidi hiyo, maana Summer ikifika utafurahi hakutokua balidi tena. Basi, usiruhusu mapito yakukoseshe raha ambazo zinakuja mbele yako kama vile Bwana alivyo sema. Simama imara, Mungu atakupigania. Ikiwa ni kwenye ndoa yako, hayo ni mapito tu, tia Imani yako na matumaini yako kwa Yesu Kristo, siku moja utapa amani na mmeo ao mkeo pia na na watoto wako. Mawazo ya Bwana si kama yamwanadamu na Njia zake si kama za mwanadamu, basi kama tunatambua hilo, lipi ambalo Mungu wetu asilo liweza? Bwana anasema yakwamba mwenye haki hatoachwa, bali humulinda na kumukinga na kumuokowa katika shida zake zote. Tafadhari mapito hayo yasikusababishe wewe kumwacha Yesu, songa mbele! Muombe Mungu akufunze kuziendea njia zake zote na kufuata amri zake, maana kuna faida kulijua neno! Mungu wetu anaitwa Mfariji wa Ajabu. Ebu tusikie Bwana alio yasema katika kitabu ya Isaya 41:9-13 "Wewe niliye kushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe Umutumishi wangu; nimekuchaguwa wala sikukutupa. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe; usifadhaike kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama wote waliona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakua si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakua kama kitu kisichokuwa, wale walio fanya vita juu yako. Kwa maana mimi, BWANA, mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume , nitakwambia; Usiogope, mimi nitakusaidia." 

Jikaze uyashinde mapito, baada ya hayo utafurahi na hutoyaona tena, Bwana ni mwaminifu kwa wenye haki! Huko peke yako katika shida hizo, Mungu yupamoja nawe! Endelea kwa maombi na Kumusifu Mungu kama vile Paulo na Sila gerezani waliendelea kumsifu Mungu ingawa walikua katika shida. Paulo alisema pia katika kitabu ya WARUMI 8:18 "Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu." Ndo maana nimesema Fall inaweza kukuumiza lakini ukifikia Summer hutokumbuka balidi (mateso) tena. Vumilia upate ushindi maana upo! Yesu alisha maliza kutuonyesha ushindi huo kwa kazi kubwa alio ifanya pale gorigota! 

AMANI YA MUNGU IWE NANYI!
The Superlative Kaburungu "Seth Vyamungu"