Friday, October 12, 2012

Fursa ya Methusela Nzisabira

Ndugu wadau huu ni kijana anaenda kwa Jina "Methusela Nzisabira" ndo majina yake kamili. Kijana huu ni mufanya miziki za nyimbo ya Injiri, anaishi apo Dallas, TX. 

Katika safari yangu ya kwanza kwenda Dallas, Texas kwa ajili ya mkutano wa Vijana (CAG Ministry Youth Conference) ulio fanyika mwezi wa 7 tarehe 7 na 8 mwaka wa 2012, na katika maandalizi ya mkutano huo, kijana huu alinisaidia kwa mambo mengi sana. Na cha zaidi na mushukuru kwasababu alinikabizia Van (gari) yake, kwa hizo siku ambazo nilikua naishi apo Dallas. Munajua ukiwa mgeni ni vigumu sana kuhusu usafiri na nirikua sina uwezo kabisa wa kukodisha (rent) gali, ila Kijana huu kajitolea ili niitumie gali (White Van) yake, namshukuru pia kwa Heshima alio nionyesha na ukaribisho wake kwa kunipokea kama mtumishi wa Mungu bila zalau wala nini, ingawa wote ni Vijana unakuta kuna maongezi furani yanamuchukiza Mungu, ila Bwana asifiwe maana kazisahau dhambi na makosa yetu. Namuombea balaka Kijana Huu Mungu amuzidishie Hekima na busara katika kazi zake zote na akumbuke kumuheshimu Mungu na kuendeya njia za Bwana kila kukichapo. 

Kwa kifupi ndungu wadau, Napenda kuwatangazia ya kwamba, kama unataka kufanya kazi yako nzuri ya audio production (kurikodi sauti), nakushauri umukabiziye kazi zako Kijana huu, maana alinionyesha uwezo wake, na katika Studio yake niliingia, nikaitembelea hata kulikodi nimerikodi nyimbo mbili ambazo nitaziweka katika album yangu ya pili. Katika miziki hiyo kijana amenisaidia kurikodi na kupiga vyombo kama Electronic Keyboard (piano), Gita (solo).  Yani hatakurikodia tu masauti, na katika mziki wa kweri nakuhakikishia kua ataweza na wewe utapenda kweli. 


Hii ni moja kati ya zile nyimbo mbili nimerikodi katika Studio yake. Mausauti ni mimi The Superlative mwenyewe, na vyombo: Base (mimi), Keyboard (mimi na Methsula, ila mimi nimecheza kasauti ambapo kanasikika kama Violin or whistle, mengine ni Methusela)  


 Hawa ni warembo katika kundi (Choir) lililotoka Abilene, TX kwenda Dallas, TX kurikodi ndani ya Studio hiyo la Methusela, inaitwa "GAP Studios -Glory Ambassadors Pro" Ivyo basi kaeni tayari Album hiyo inakaribia kuafikia endapo makandamizi yakimalikiza. 


Nafikiri mnamuona na yeye kwenye mtambo ya mziki akiwa na gita (amevaa rangi ya blue, In blue behind the guy in red) 


Kama kawa akiendelea. Kijana anaejiita "Dr. Pastor Eric" mtunzi (Owner and Operator) wa website ya www.africamusicproduction.com, uwo kwenye upande wa kushoto akikaa amejishangaza sijui kashangaa nini! hata na yeye alikuwepo akisikiliza makatandamizi ya kwaya hiyo. Na wanakwaya naona wakapa mapozi kidogo, ao sio. 

Basi nitajitaidi niwajurishe mkanda (CD) ikiondolewa ili nanyi mujipatie raha. Tafadhari tuwe tunasaidiana Jamani. Wenzetu wakifanya mambo, basi tununue ili tupate kuendelea mbele, na tuhakikisheni tumenunua Original Copy.