Friday, April 29, 2011

21Days Ipo madukani sasa. Pateni nakala zenu...


Basi ndugu watazamaji hatimae 21Days yaingia sokoni. wadau wangi walikua wakinipigia simu na kunitumia messages wakidai ni lini movie itaondolewa, nami nilikua nawajibu kua bado kweli filamu ingali inahaririwa na kuchunguza kama kweli tutaondowa kitu bora. tulikua tunahakikisha ila filamu iwafikie ikiwa bora. basi japo imechukua mda kidogo filamu kwa sasa ni yenu, jipatie original copies.  

Tuesday, March 15, 2011

Movie yenyewe ni hiyo


Hii ni front cover ya 21Days movie. wadau na mashabiki naweza tangulia shukurani kwa Mungu, naimani filamu itawafurahisha japo kuna mabadiliko kidogo yametokea. katika shooting, kikosi cha B-Squad kutoka New York walitutembelea kwa kusaidiana na ku support. Filamu imeshafika ndani ya Afro Shemeza Studios kwa uhariri muda sio mlefu mzigo unaondelewa. basi kaeni makini mujitayarishe mezani kwani chakula kinakaribia kuwafikia na mutaniambia wenyewe. 

Johnson Mukubwa kwa mala ya kwanza yeye kucheza filamu, anasema hakutegemea angefanya alivyo onyesha katika filamu hiyo. Mwana dada Irene Kasongo (in cover), naye kafumua zake na kuwapa burudani ya kweli bila utani. 

Friday, March 11, 2011

21Days inavuma ngoma

Wadau 21Days inakaribia kuingia studio kwa uhariri, The Superlative nikawa naitendea haki. apa nikawa na shoot moja scene katika filamu hii.

Uyu ni mama Kamikazi katika moja ya scene in movie, akawa anapata maelezo ya kufanya. Mama huyu ameonyesha uwezo yani apa atawapa burudani. sipendi nimusifii kwa sasa ngojeeni mzigo utoke mutaniambia.

Mwana dada  Yvonne Ndayisenga ''Shenaiza'' ameingia katika tasnia ya UGLEAWOOD Movies, hapa akiwa tayari ku shoot movie. subirini awape zake huo mwana dada. 

Wadau huu ni Johnson Mukubwa anasema kua anaenda kua bega na mimi mpaka anawaonyesha uwezo wake, yani kwanzia leo ni swahiba wangu. ndipo akapenda ni mupe nafasi ya kuonyesha uwezo wake yani apo ametoka Canada mpaka USA. wadau nimependa uigizaji wake hadi mwenyewe sikutegemea kua angefanya nilio yaona. kueni hewani mzigo unakaribia kuondolewa. 


Wednesday, March 9, 2011

Ndugu wadau nakaribia kuapa mzigo wenu, mimi hapa nikiwa katika maandalizi

Wadau na wapendwa wote kama nilivyo wa aidi kama nitakua nawa blog na kuaeleza kazi zangu, basi huu ni mimi mwenyewe The Superlative nikiwa Boston, MA ndani ya Mall apo mchezaji wangu mpya Nyandwi zebedayo ''Robot'' akawa amenipeleka mitaa mbali mbali kwa maongezi zaidi ya filamu. Kijana huu anachekesha, kwa maongezi yake utakutwa umesha sahau na kile ulicho kipanga kufanya na amenihakikishia kua anaenda kuonyesha uwezo wake hasasa baada ya filamu hii.  

Apa ni mimi na mchezaji mpya Nyandwi Zebedayo ''Robot'' (left-kushoto) yani baada ya maongezi tukaon vizuri twelekee nyumbani ndipo sasa kidogo tukachukua ma pozi. 

Ndugu wadau mzigo huu unaenda kuwapa burudani na sipendi nijisifie ao nisifie filamu kabla hijaondelewa, wenyewe mtaniambia mzigo ukisha kua mitaani. kaeni kwamakini nitawapa Surprise week hii.


Wednesday, February 23, 2011

21Days inakalibia muda sio mrefu...


Napenda kutangulia kuaomba radhi siku nyingi sipatikani kwa blog hii, nilikua bado na burudika na mapumuziko pia na kazi zingine ila naona mapumuziko yameisha narudia kazini rasimi na muda sio mlefu movie murikuwa munangojea muda mrefu sana basi itaondolewa mwezi huu wa tatu (March). 


Basi mutajiuliza mengi kuhusu movie hii 21Days kwanini commercial ya kwanza na cover images haiko kama leo? ki ukweli wadau,  nilipenda niwape burudani ambao itawahakikishia kua mwenyewe The Superlative kazi naiweza na sio muchezo. nimeibadilisha kabisa iko mupya na tena kwenye kiwango cha hari ya juu.  naimani wadau wengi hapa USA & Canada mutaipenda sana. wechezaji ni wapya sijawai kuwatumia ila jinsi navyo waona kuweni tayari kuwapa ufunuo wa filamu. siwezi wasifia kwa sasa, napenda muitazame kisha wenyewe mutaniambia. 


Ndani ya siku chache nitawaonyesha Cover mypa ya Movie hii, na Movie Trailer. 
Kueni makini nimerudi apa blog nitakua nawajulisha kinacho endelea. 


Bado inatayalishwa na Afro Shemeza Studios (UGLEAWOOD Movies, www.ugleaworld.ning.com)



Tuesday, February 1, 2011

''Uruwo Gushimwa'' Album


Hello fans, Just reminding you about my First Album ''Uruwo Gushimwa'' which gives me a honor to pray or worship the Lord. Thanks to those who give me congrats for it and I really do appreciate it a lot. 

So if you haven't listened to it take a chance to visit my Youtube Channel at www.youtube.com/vyamungu25 or win a free CD when 21Days comes out. 

Friday, December 31, 2010

Mwaka mupya na mambo mapya.

Ndugu wapendwa pamoja na wadau wangu wote, nashukuru kwa musaada wenu kwa kunipa matumaini kua nitaendelea vizuri. Pia na toa shukurani kubwa sana kwa Mungu alie sababisha haya yote nakunipa uwezo wa kutenda haya yote, na namuomba mwaka huu wa 2011 uwe mwaka wa mambo mapya na balaka zaidi. 


Tunashukuru Mungu anaye tupitisha katika mwaka unayo pita, kweli kabisa tulifanya mengi japo shetani aliharibu ila Mungu anatupigania siku kwa siku. jamani mwaka mupya na mambo mapya. sasa tugeuke tuwache ujinga wa mwaka ulio pita tuka anze na mwaka wa 2011. nahisi kua huu mwaka utakua mwa muziri sana kwa kua na anza maisha upya tena na badaliko pia na balaka za Mungu. Nashukuru Mungu kwa hilo.


Katika kuigiza kwangu, naomba Mungu awe mwanzo kwa kila jambo nitakalo lifanya. filamu zangu zikawafundishe yalio mema na kuepukana na mabaya. Na aidi wadau wangu na mashabiki na ndugu wapendwa kua movies zangu zinaenda kua bora zaidi na quality ya hali ya juu. na kwa kuaonyesha ivo nimewawekea community (UGLEA World Community - ugleaworld.ning.com) kuwaonyesha kua tunaenda kushirikiana na wa artists wote kwa pamoja tukawape burudani. movies zangu nyingi tena bora zaidi zina karibia. nitafurahi sana wadau mukinisaidia kwa kununua na ku support.


katika kuimba kwangu, nafurahi tena kwa vile na muimbia Mungu. naimba Gospel Songs and Worship songs. mala kwa mala utakuta na rap ila maneno ni mungu. wadau nyimbo zangu za mwaka huu ziwafundishe na mupate balaka Mungu akawasaidie sana katika mambo yote munayo fanya.


huu ni mwaka mupya na mambo mapya. kama unahisi kuna kitu unataka kufanya ila huna uwezo. usi site kuniita tukasaidiane. nipo kwalo njo pamoja tumwombe Mungu atupe balaka na mafanikio. huu ni mwaka mupya na ningependa wote tumukalibishe Yesu kua mwokozi wetu wa maisha yetu. kama una shida una kitu unataka kufanya ila shetani amekutenga nacho, na unaitaji musaada wa maombi, karibu nipo muda wowote, njoo tukamwombe Mungu naye atatenda! 


Asanteni nyote nawatakia mema katika mwaka huu wa 2011


-The Superlative Kaburungu-