Thursday, November 1, 2012

Burundian Gospel kuanza kazi rasmi, Fursa mpya ya mziki wa Mungu kwa warundi

Nimeanzisha Kampuni Mpya "BURUNDIAN GOSPEL". Kwa siku nyingi nikiwa naongea na wadau wangu, hua wanadai yakwamba hakuna Entertainment katika kazi ya Mungu. Hasasa nikiwa naongea nawale wanaojifasha ni wasanii ambao wanaimba nyimbo za mapenzi hua nawashauri ili tuweze kumutumikia Mungu ila wakadai yakwamba katika nyimbo za Injili hakuna Entertainment. Basi ndugu wadau nimeanzisha rasmi Kampuni ya BURUNDIAN GOSPEL Entertainment ambao itatangaza nyimbo ya Injili na kusambaza kazi za waimbaji. Unapewa karibu kama wewe ni mrundi ambao unaimba nyimbo za Injili na unataka kazi zako zisambazwe na kuuzishwa. 

BURUNDIAN GOSPEL inasaidia watu ambao wanamuimbia Mungu (nyimbo za Injili), kama wewe ni muimbaji tofauti na Injili basi BurundianGospel haipo tayari kukusaidia kwa lolote na  samahani sikwamba tunauchaguzi ao upendeleo ila maono yetu nikwamba kazi ya Mungu isonge mbele. 

Na kwa hivyo sasa naenda kuanza kazi na studio yangu Afro Shemeza Studios (Audio & Video Productions), niko najiandaa kununua vifaa vipya na siku si nyingi nitawaonyesha vifaa na mengi mutakua munayajua kwa site hii ya www.burundiangospel.com". Siku si nyingi nitawajulisha nyiye nyote ambao muna ma band ao choirs, Videos na Audio zenye aina yake zinakaribia kuwafikia, itakua ni bahati yako kuitumia kampuni yangu ya Afro Shemeza Studio. 

Nataka nitoe shukrani zangu kubwa kwa Emmanuel Irankunda AKA "Lil Ace". Kijana huu amenifsaidia sana katika utengenezaji wa burundiangospel.com site. Kwa uhariri na utengenezaji wa hari ya juu kuhusu website yako nakusihi umupe na fasi kijana huu akutengenezee maana yuko juu. Na katika jamii yetu (Burundian Community) ya kisasa kwa warundi tunaitaji watu kama hawa ambao wako tayari kutusaidia katika mambo ambao hatuko tayari kukamirisha. Usikae nyumbani Kijana yote yule, nenda shure ao tumia kipaji chako ili mambo ukaweze kua kitu muhimu katika maisha yako na jamii. Mungu ambaliki Kijana huu, na tafadhari shirikiana nami kwa maombi kwa kumushukuru kijana huu na kumuombea balaka katika maisha yake. 

Nndugu wadau hizi nina kampuni tatu zinaenda kutumia kwa pamoja yani kama kolabo: "BURUNDIAN GOSPEL", "Afro Shemeza Studios/Stores" na hizo zote zifunikwa na kampuni yangu kubwa sana ambao natarajia kuingiza katika jamii yetu, nayo ni hii "The QLS, Inc. -Quality Life Solution-. Kwa siku chache nitawajulisha habari nyingi kuhusu Kampuni hii, na hakuna kampuni nyingine ambao nafikiri nitafanya maana izo tatu zinatosha, nataka kwanza niziinue. CAG Voice Entertainment imefinikwa na BurundianGospel Entertainment; msije mukashangae kwanini siitumii tena. 

Basi nawaalika ngudu zangu kua mnatembela www.burundiangospel.com mala kwa mala kwasababu tutakua tuna post mambo mapya kila kukichapo. Tembelea na uwaalike ngudu zako ili kazi ya Mungu iendelee mbele! 

Amani ya Bwana awe na nanyi!
The Superlative Kaburungu