Thursday, September 6, 2012

Pierre Lukata AKA Young PDK

Picture taken in interview with The SYUB Show

Kijana wenye Heshima zake Pierre Lukata ambae anajulikana kwa Jina la “Young PDK” Kijana huu amefanya zake za kuinua Industry ya warundi apa malekani na Inchi mbalimbali za Nje. Pia ni Pruducer wa SYUB Show akishirikiana na Steven Raphael wakitesa apo Houston, Texas.


Young PDK ni Founder and Chair man wa EASTAFRICANHIT.com website hiyo inatangaza habari mbalimbali za wasanii wa warundi na watanzania. Young PDK ni mrundi ambae amezaliwa nchi ya Congo. Katika SYUB Show aliaidi ya kwamba hata waimbaji wa Nyimbo za Njili anawapa karibu awatangazie kazi zao katika website yake. Tembelea website EASTAFRICAN.com utapata kujua mengi kuhusu yeye.

Akiendelea na pozi mbalimbali baada ya Show, nafikiri alikua ana check jinsi Interview ilikua.

Warundi, tusaidiane katika kazi zetu ili tuyiendeshe mbele Nchi yetu ya Burundi. Naimani kuna mabadiliko yanaenda kutokea kwetu sisi warundi hapa malekani tukishirikiana kwa upendo na umoja!

The SYUB Show

MH. (Mheshimiwa) Steven Raphael, nisinge muita kijana maana ana famalia ndo maana nikamuita Mheshimiwa, kwasababu napenda kuwaita ivo walio jenga familia zao.


Steven Raphael ameanzisha Show inaitwa SYUB Show (Sauti Ya Uwamusho Burundi) show hii inakutaarifu kazi za warundi zinazo fanyika apa USA. Show hii inapatikana katika mtandao wa YouTube, ni mda wako sasa wakusikiliza. Tafadhari warundi tusipuuzie maana hii ni moja wapo wakuiendelesha mbele kazi na taifa ya warundi Nchini malekani. Ni waajibu wako sasa wakujua habari tofauti za warundi hapa USA na Nchi zinginezo za Nje.

Kama una Business unataka kutangaza, na unapenda ijulikane watu wakuelewe wewe ni nani, unafanya kazi gani, una mpango upi wa kuinua taifa la warundi, karibu uwasiriane na Steven Raphael kwenye facebook utampata na mtaongeya mengi.

SYUB Show ipo tayari kuinua Burundian Industry apa malekani, karibu uwatembelee kwenye YouTube “The SYUB Show”. The SYUB Show inapatikana Houston, Tx. Kwa mengi zaidi nitawajulisha endapo munaendelea kunitembelea katika blog yangu hii. 


Hii ni Crew (group) ya SYUB Show, kulia ni Willy "SYUB Camera man", katikati ni Steven Raphael "SYUB Representative and Director", kushoto ni Pierre Lukata AKA Young PDK "SYUB Producer and Editor" kuna mwingine ambae haonekani katika picha hii, Celestin Niyongabo "SYUB Camera man.