Tuesday, October 9, 2012

Je ni kweli Maisha yanachanganya?

Sababu yakulinga, tumwo ndani ya Yesu, sikiliza tafandari usipuuzie. Naomba pia ukisoma apo chini uwezi ku Comment, ili umubaliki mwenzako atakae soma hii. Unaweza hata kuongeza maoni yako, utabalikiwa kwa maana utakua umewasaidia na kuwafurahisha wengi wanao sona Ujumbe kutoka blog yangu hii. Asanteni! Haya, tusome sasa, ...


Ndugu zangu katika Jina la Yesu, hua kuna swali Vijana wengi tunapendelea kuuliza ao kusema. Je Maisha yanachanganya? Vijana wengi wanadai yakwamba maisha yanawachanganya ndo maana wanaangaika uku na kule ili wapate maisha. Wengi hukimbilia katika usanii kuimba nyimbo za kisanii, na wengine hukimbilia katika sanaa (movies), wengine wanadhiriki hadi kufanya kazi mbili au tatu eti apate maisha bora, na hapo kanisani haudhurii. Unakuta na wengine wanaendea njia nyingi eti mladi wapate maisha. 

Nisikilizeni enyi wote vizazi vya Mungu, Maisha hayachanganyi ila sisi ndo tunayachanganya na kujichanganya wenyewe. Unakimbilia kuimba nyimbo za kisanii, unamsifu mwana mke ao mwana mme badala ya kumusifu Mungu. Na katika huduma hiyo, Vijana, nawatangazia yakwamba hakuna mafanikio hata siku moja. Ni hakiri gani kumsifu mwana mke ao mwana mme ambae ni mavumbi kama binadamu wengine? Kisha faida gani utakao itoa kutoka katika huduma hiyo ya kumusifu? malipo gani umepata kutoka kwake? Hamna, tena haitowai kutokea mwanadamu kurizisha moyo wako hata siku Moja. Pia mnajua yakwamba, "amelaaniwa amtegemeae mwanadamu" ndivyo munavyo Jiletea laana na mikosi katika huduma hizo, baadaye mnalalamika eti maisha yametuchanganya, tunajaribu kuyatafuta huku na kule. Maandiko katika kitabu cha mwanzo (Genesis 1:28-29) yanatwaambia yakwamba baada Mungu kuumba mbingu na Nchi akamwumba mwanadamu, alisema pale mstari wa 28, zaeni mujaze ulimwengu wote, nawapa kumiliki vyote vilivyomo ulimwenguni. Na hayaishii hapo tu, baada ya pigo kali wanadamu walio pata enzi zile za Nuhu, Bwana alimwambia Nuhu na kumwaidi vile vile kua hatoangamiza tena binadamu kwa maji, na akamwambia kua watamiliki wanyama na vyote vilivyomo ulimwenguni (Genesis 9: 1-3). na tukumbuke sote tulizaliwa baada ya hao. ] Kama Mungu alisema hivyo, waweza kusemaje yakwamba maisha yamekuchanganya? Mungu alie kuumba anazo sababu za kukuumba wewe pia anayo huduma yakutosha ili akutunze. Kama angeshindwa kukutunza hange kuumba, ungekua umefariki kama wale watoto wadogo wanao fariki wakiwa wachanga sana ao hata kuzaliwa hungezaliwa. Ila kwasababu ameona kua anao uwezo wa kukutunza ndo maana akakuacha ukakua Ila umekua na ukabadilika. Nilikupanda uwe muzabibubu mwema, umegeukaje kua mzabibu mwitu? Bwana kasema (Jeremiah 2:21)! Tukiendelea pia kusoma maandiko matakatifu katika kitabu cha Jeremiah 4:18 panasema yakwamba "Njia zako na matendo yako ndo yamesababishia hayo (magonjwa, mkosi, mapigo, shida, etc), huu ndo malipo ya uovu wako. Ni kweli ni uchungu tena yanafikia hata moyoni mwako)."Tukiendelea kidogo kwenye msitari wa 22, Bwana alisema: "Watoto wangu ni wa pumbavu, hawanijui wala hawajui njia zangu. Wana hekima ya kutenda maovu ila hekima ya kutenda mazuri hawana." Jiulize sasa mwenzangu, bado walalamika eti Maisha yanakuchanganya? Ebu tusilikilize maneno Yesu alio sema katika kitabu cha Yohana 8:12 akiwa anaongea na wafarisayo, akasema: "Mimi ni nuru ya ulimwengu, na yeyote atakae nifuata, hataona giza kamwe (Giza inahesabiwa kama Magonjwa, shida, majaribu, mikosi, uhalibifu, etc). Badala ya hayo, atairidhi Nuru ya uzima wa milele." Hii inatuhakikishia yakwamba kumfuata Yesu ni kupata maisha yario bora pasipo shida na majaribu. Sasa wewe kama mkristo, kwanini unakutana na hayo? Jamani tusimulaumie Shetani, maana sisi ndo tunamtafuta badala ya yeye kututafuta. Biblia inatuweka wazi jinsi ya kujilinda na ule mwovu. maandiko yanasema katika kitabu cha Jacob 4:7 neno linatwambia "Basi mtii Mungu.Mpingeni Shetani, naye atawakimbia." ukiendelea katika mstari wa 8, panasema: "Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu enyi wenye nia mbili. Tukisogea kidogo pale kwenye msitari wa 10 panasema: "Jidhirini mbele za Bwana, naye atawakuza." Tuseme nini sasa Vijana! Unataka turudie tena kuawambia amri za Mungu. Shetani ukimukaribisha atakuendesha kweli kweli, ubaya wake anakuendesha kama gali mbovu, hujui niwapi maisha yako yanaelekea, ndo maana unahangaika. Yesu ndo mwanzo na mwisho, pia ndo funguo ya maisha. Hakuna aliye kuja kwake akaadhirika wala kupata shida. Alituaidi yeye mwenyewe katika kitabu cha Yohana 10:27-30 Yesu akasema: "Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami huwajua, nao wanifuata. nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakae wapokonya (yani kuwatoa) katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni Mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa baba yangu. Mimi na baba tu umoja." Kijana ao mtu yeyo unaye sikia maneno hayo, hivi unajiuliza nini ao unangoja nini kumpa Yesu maisha yako. Maisha hayatafutiwi katika hanasa za dunia, wala katika tamaa za myili yenu; amna kabisa, maisha ni kwa Yesu pekee, yupo tayari kukusaidia. Waweza kuniuliza; mimi sina Yesu wala mambo kama hayo, mbona naishi vizuri. Jibu: "Mambo yote ya dunia hii yatapia, ila neno lake Bwana ni uzima wa Milele" Ebwana we, hata Shetani anawasikia walio wake na kuwapa maisha ya mda kitambo tu, jiulize kwanini ameleta AntiKistro! Wewe unakaa apo eti unamwabudu Mungu, kumbe unamwabudu Shetani; hua na yeye maombi yetu anayasikia, kisha Antiskristo akifanya kazi eti Mungu kanijibu, tafadhari pima kua Jibu zote zimetoka kwa bwana (1John 4:1-6), wakristo kaeni macho. Kijana kama unavimba, vimba na Yesu; dunia hii siyakwako. Msichana kama unalinga, linga na Yesu; dunia hii siyakwako. Hata na sisi tunaweza kua wasanii tena kuazidi, ila yote tunayafanya kwa mapenzi ya Mungu. Usijivunie mali wala vipaji kaka na dada zangu, ila Jivunie Upendo na neema za Mungu tunazopewa Bure, Mungu kasema hayo katika kitabu cha Jeremiah 9:23. Ulimwengu tunapita, wote tutaozea kaburuni bali walio mfuata Yesu, hawata shududia kifo hata kidogo, maana kifo ni njia yetu yakwenda Mbinguni. tutamraki Bwana mawinguni. Malipo yote nihapa hapa duniani. Bwana ataturipia hapa duniani wema tulio ufanya, kisha taji ya uzima wa milele uko mbinguni. Kwenu nyiye mnao jifanya niwakristo kumbe amri za Bwana hazipo miongoni mwenu na ninyi wenye dhambi, malipo yenu ni hapahapa ulimwenguni kuteseka kisha baadaye kufia jehanamu kwenye moto wa milele. 

Nashangazwa sana na watoto (wasichana na wavulana) wa wachungaji. Ikiwa baba yako ni mchungaji, Mwarimu ao cheo furani kanisani, Jamani nyiye wanao mumebadilika sana. Bwana Yesu alisema pale katika kitabu cha Yohana 5:19 yakwamba hakuna chene mtoto anafanya pasipo kuiga babae, maana babae humufunza njia zote za haki." lakini vizazi vya leo badala ya kufuata tabia na nyendo za wazazi wenu (wachungaji, etc), nyie watoto wa wachungaji mumekua kelo kwa wazazi wenu. Wengi ni wasanii, wakahaba, kuvaa nguo za aibu, tabia chafu na mengi zaidi yakufanana na ndambi. Katika kitabu cha Mithali sura 30:11 panasema yakwamba: "Kuna vizazi havieshimu baba zao, na wengine hawabaliki mama zao." ndo mulivyo katika ulimwengu wa sasa. Neno la mungu linasema: "Waheshimu baba na mama ili uridhi Nchi Bwana aliye kupa, na amelaaniwa atakae tukana wazazi na kuwazalau ao kutokusikia ushauri wao." Jiangalie usije ukakute kumbe umelaaniwa zamani. Nuhu alimulaani mwanaye kwakunchungulia uchi wake, natena laana ilimushika kweli kweli (Genesis 9:18-27). Ndo maana utakua unafanya mambo na hufanikiwi, wazazi wako wanakuombea ili umurudilie Mungu, nakwambia wazi hutokwenda popote; ni mambo haya mawili: utakutana na shida kisha kifo, ao mwisho wake utamukumbuka Bwana."  Basi, kumbukeni mulipo anguka na mukatubu makosa yenu. Yesu yupo tayari kuwapokea na hatowaacha kamwe! 

Tembelea www.kaburungunews.blogspot.com na usipuuzie, pia usitazame sanamu tu ila soma maandiko na utabalikiwa. Mpeane Ujumbe huu kwa wenzenu wote mnao jua, mutabalikiwa na Mungu.