Romans 7:14-25, Hebrews 12:1
Ndugu wadau, nawasalimu wote kwa Jina La Yesu! Huu ni wimbo nilio aidi wadau wangu kua nitawatilia kwenye Youtube kabla ya kuondoa album. Nime aidi nyimbo mbili tu, ila kwanza nawatilia huu, mwingine nitatia badaye. wimbo huu nimeurikodi katika studio ya Methusela Nzisabira (GAP Studio "Glory Ambassadors Pro Studio") mjini Dallas, Tx. Baada ya mkutano mwezi wa 7 mwaka huu wa 2012 nikaona nitembelee studio ya Kijana huu kama mrundi mwenzetu na tangu apo tukawa marafiki na kuanza kuongea mengi kuhusu utengenezaji wa Audio. Vyombo katika wimbo huu vilipigwa na mimi pamoja na Methusela nzisabira, masauti yote ni mimi mwenyewe Kaburungu. sirikilizeni na mujifunze.
Utumwa katika wimbo huu nikwamba mala tunakutana na majaribu mengi na mambo yanao tuzuwia kuifanya kazi ya Mungu, kama facebook, simu, Internet. Wakristo unakuta tunatumia mda wote wetu kwa mambo hayo badala ya kusoma biblia na kuomba, kufunga (maombi) na kumuheshimu Mungu. Kile tunacho taka kufanya sicho tunacho fanya. Tamaa za mwili zimetuteka. Wengi tulibadilisha maumbile yetu, wengine tunavaa nguo zisizo pendeza (aibu mwanamke kuvaa suruwali, nguo kama mini, hereni na mengeneo hivi ya kufanana), wengi tunadai yakwamba Mungu anaangalia moyo pekee ila anaangalia vyote ( Ezekiel 44:9) kuingia katika ufalme wa mbigu ni razima uwe safi mwilini na moyoni. Si hayo tu, kuna ukahaba, uzinzi, uongo, umbea, ujambazi, mambo ya kisani, na mengi ya kufanana na dhambi. Ni bora tujiepushe nayo maana tumesha tekwa na minyororo ya shetani kama vile anatuendesha kama gali mbovu. ni vizuri tujiangalie mambo tunayo yatenda tusije tukajikuta ni watumwa wa shetani. Wewe kuimba, kuhubiri, kufanya kazi furani ya Mungu haikufanyi kua uko msafi, kama bado una tendo la kufanana na ndambi bado wewe ni mtumwa wa shetani. Tumefungwa na tamaa za mwili ndio maana hatuwezi kuona ni wapi tunaelekea pasipo kufungua macho ya kiroho tujue ni wapi tumekosea na tumurudilie Bwana. Mafanikio na mazuri yatakua mbele zetu ila matendo yetu mabaya ndo yanatusababishia mikosi, magonjwa, laana, shida mbalimbali (Jeremiah 4:18); ndo malipo ya ubaya wetu. utavuna ulicho panda ndugu yangu. Tutambue na Shetani (kutumia Antikisto) anafanya miujiza, si kila jibu lote limetoka kwa Mungu, tafadhari jaribu kwanza ukajue jibu limetoka wapi. Unapo omba shetani huwa anasikia maombi yako, badala ya Mungu kukujibu shetani atajipendekeza ili aweze kupata njia ya kukuharibu. Ndo badaye sasa utaanza kulalamika eti kwanini Mungu amenijibu na ikaharibika ao ikageuka kua kikwazo? Mungu akijibu anajibu wala hakuna mabadiliko, tukimtii na kuziendea njia zake zote za haki, mkono wake utakua nasi milele daima. Ni vyema sasa ujichunguze vizuri mala kwa mala ili uhakikishe kabisa unatembea katika mapenzi ya Mungu.
Burudikeni na wimbo huu, pia muniombee ili Album nije niitoe salama. Kama unataka kusaidia, msaada pia unaitajika. Ikiwa ni kwa maombi ao kwa kila kitu chochote kile, kikitokea moyoni mwako, Tuatabalikiwa wote. Tusisikilize tu bila kujifunza, bali tusikie na tujifunze, maana Yesu alisema heri anaye sikia na kutenda (Kusikiriza na kutenda). Tuambiane pia tushauriane wote, kama umefanikiwa kusikia wimbo huu, basi utangazie kwa majirani na ndungu na Jamaa utabalikiwa, maana utakua unaitangaza Injiri ya Bwana kama vile alivyo sema; "Enendeni Muyageuze mataifa yote kua wanafunzi wangu! mujuwe hili: nipo pamoja nanyi siku zote, hadi siku za mwisho" Yesu kasema!
Mbalikiwe
The Superlative Kaburungu