Wadau wengi hua wanasema hii nyimbo ni ya mapenzi, labda kwasababu mwendo wa nyimbo unafanana na Hip Hop ao kama nyimbo za kisani. Kipaji nilicho nacho naweza kuimba katika Style yote ile ingawa si style zote ila nimefanikiwa kuimba katika style nyingi. Hii wimbo si ya mapenzi ila ni ya kushauri Jamii: "urukundo nagukunze ngo tubane amahoro, ariko ukampora uwo ndiwe, ubwoko nakaranga." Katika jamii zetu za kisasa watu huzarauwana ao kuchukiana kutokana na ukabira wa mtu ila sisi wote tumeumbwa na Mungu mja. uwe muisilamu, uwe mukristo, uwe na dini gani ao kabira ipi, ujuwe yakwamba sote tumeumbwa na Mungu mmoja alie hai, Muumba wa mbingu na Inchi maana Dunia na vilivyomo ni mali ya bwana. Tupendane, tusichukiane, kama Nchi zetu za Africa, tuwe na umoja katika maendeleo ya kimaisha. tusibaguwane wala tutengene, tujue upendo wa Mungu jinsi alivyo tupenda bila upendeleo, anamwinua anaye mtaka na anamushusha anaye mtaka. Mawazo yake na njia zake sikama za mwanadamu. Basi tufuate mtindo huo wa Yesu.
Naimani tumeelewa ya kwamba wimbo huu si wa mapenzi ao nini, ila ni ushauri kwa Jamii zetu. Walio kua na maswali na Imani mmelizika na nawashukuru kwa support yenu na maombi yenu ili kazi ya Mungu iendelee, tuendelee kupendana hadi mwisho wadunia.
Mungu awape balaka na Hekima
The Superlative Kaburungu
No comments:
Post a Comment