Wednesday, February 29, 2012

Tafadhari ndugu wadau tuwe tunaelewana!

Wadau, kuna mdau ali post comment kwenye wimbo wangu ''Uruwo Gushimwa'' kwenye Youtube akisema hivi, hii ndo comment yake: 
''Nawe vyarakugoyepe! mara Urimumamovie,Mara Mumiziki, Mara muvyimana.
Dufatiki Tureke Iki? ndabaza.Uragahungarema rero ntakundi twabisigura.
Njia mbili zili mshinda mzee fyisi.basi kwarukubazagusa.murakoze kutugezahi.Deney U S A.'' 

Jamani nimefananishwa na Popo! kwa kiswahili uwo jama amesema kua mala nasikika kwenye nyimbo za mungu, mala katika ma filamu, pengine kwa wasanii, eti je ni upande gani nilipo ao niko kama popo? 

Jibu:  Ndugu, jamaa, na mashabiki kama unawazo kama hilo, nataka tuelewe kua kila kipaji kina faida yake. Sijui huu mdau aliona nyimbo nime imba pamoja na mdau wangu Remejio ambae anaishi Seattle, WA; ile wimbo haikukua lengo langu kuiimba! Remejio ni mmoja wa wadau wangu uko Seattle; huu naye ni mmoja kwa walio nipa nguvu kwa kuendelea kazi zangu na kufika mahali nilipo leo. August, 2011 alipenda niimbe wimbo pamoja naye wa kumbukumbu maana nilikua najiandaa kuhamia Hawaii. Ndipo akapenda tuimbe wimbo kuhusu wasichana na akataka nimfanyie video ya wimbo huo. Apo sikukua tayari na vyombo vyangu ili ni mu shoot vyema, ila nikatumia simu tu na jama akashukuru sana kwa hilo. 

Nakama ni Rap kama wimbo ''N'umparire'' ''Oh Dunia'' Jamani Injili ya Mungu haina limit kwa style. Watu wengi hasa warundi, wanajifanya kua niwa kristo sana tena kisana. Nataka tujue yakwamba kila kipaji chochote kile kina faida yake. na kama ni filamu, tujue kua filamu ni moja ya ushauri tena unao badilisha wengi kutokana na ushauri uliyomo ndani ya filamu hiyo. filamu si mbaya, mwanadamu ndo mbaya. kama kuna usherati ndayi ya filamu, haimufanyi ule alio icheza kua msherati, bali ni mashauri wanatoa ya kwamba usherati ni dhambi. Basi kama alio cheza sanaa hiyo ni msherati, hiyo haitasababisha pia kua hiyo filamu ni dhambi ao walio cheza ndani ya filamu kua wote ni washerati. hilo tuelewane. Mimi ni mhubiri tena mtumishi wa Mungu. Neno la bwana linasema hivi: ujihadhae usijifanye kama wewe ni mtakatifu wa sana.'' apo mwenzangu utakua umepotea. Wote tuna tenda dhambi, isipokua tu ukiungama dhambi zako, Yesu ataziosha. 

Tukumbuke mfalme Dawidi kabla ya kubalikiwa kua mfalme, alikua mchunga kondoo. Kipaji chake  alikua akigombana na simba na vingine kama ivyo; ulipo fika wakati goliati akawadhihaki wana Israel eti nani wa kusimama agombane naye? Watu wazima kabisa wakashindwa hata kumsogelea tena walikua na vifaa vya vita ila walishindwa kumsogelea. Kijana mdogo ''Dawidi'' kwa kipaji chake cha kulipua manati, aliweza kumuua Goliati! Jamani vita si vya mwanadamu ni vya Mungu, na kipaji ni balaka za Mungu! kila kipaji kina faida yake. Nami nitatumia kila kipaji Mungu amenipa kwa kumpa heshima zake, ikiwa kuhubiri, nyimbo kwa Rap and Injiri style, filamu, video shooting, editory, design, na mengineo, mimi nitaieneza Injili ya Bwana. Na kama unaona si vyema navyo fanya, basi nikuombe usi nihukumu usije ukahukumiwa mwenyewe. Maana hata na wewe huyajui uyatendalo! kikubwa niombee na nikuombee ila tusi tusane ao tuhukumiane! Tusome neno la Mungu na Tuelewe. 

Asanteni 

The Superlative Kaburungu ''Seth Vyamungu''