Wednesday, December 26, 2012

Heri siku kuu njema kwa wadau wote!

Ndugu wadau, nawasalimu katika Jina lake Mwokozi wetu Yesu. Napenda nitangulie kumpa Shukrani za thati Mungu anaye tuwezesha katika maisha yetu ili tuweze kufika mahali tulipo. Kama navyo pendelea kusema yakwamba, Hivi nilivyo mimi kwa leo, nikwaajili yake Yesu, kama nina vipaji mbalimbali, nasikika ulimwenguni, si mimi bali ni Yesu ndani mwangu anaye tenda kazi na ni yeye mwenyewe anaye yafanya yote, mimi sina ujanja wote ule! Utukufu, Heshima, Shukrani na Sifa vimurudilie yeye "Yesu". 

Katika kumalizia mwaka huu, Namwomba Mungu anipe nguvu na vipaji mbalimbali katika mwaka mpya ambao tunaenda kuanza wa 2013. Mwaka wa 2012 kweli nimeona mkono wa Bwana na ulikua mwaka wa mibala nyingi sana katika maisha, sikua kua kama nilvyo ao kutenda kama nilivyo tena. Namshukuru Mungu ameniwezesha nikafanya mkutano wa Vijana (CAG Ministry Youth Conference) kwahiyo Mungu apewe sifa kwa jinsi ametuezesha na si hayo tu katika mwaka huu kweli ametenda mengi, kuanzisha kampuni mbalimbali kama BurundianGospel Entertainment.  Na kundi ambalo limekuja kwa muvutio kali "UBS Gospel -Himbaza Collection Vol1-" kweli Mungu ni wa ajabu jinsi anavyo tenda kazi zake. Ndugu wadau, Mungu tukimpa nafasi ili atende ndani yetu kweli atatenda na sisi tutalizika. Tatizo hatuna mafanikio, hatuitaji kumpa nafasi pia na kumuheshimu. Maana Mungu hukaa katika Heshima na Sifa. Kinyume na hayo, Mungu hutomuona kabisa. Kumshemu ni kumusikia na kutengana na dhambi maana unajua yakwamba anayachukia hayo. Na katika Sifa, kumbuka kumshukuru maana yeye ndo anatenda, sisi ni vyombo tu.  

Basi kwa mwaka huu wa 2013, labda nisitaje eti nitafanya nini kwasababu nangojea matenda ya Bwana. Kuna ahadi zake njema tena nyingi kabisa na hizo zote mwaka wa 2013, mutaziona endapo tuaendelea kuombeana ili ule mwovu asije akajitokeza kwa majaribu yake. Nawatakia siku kuu njema, Mungu awazidishie balaka, tumalize mwaka salama na tuanze mwaka mpya kwa usalama pia. Kikubwa zaidi, tukumbuka kumshukuru mwenyezi Mungu alie tutendea ili tufike mahali tulipo, maana sisi binadamu hatuna ujanja, hesabu ya siku zetu za kuishi zimo mikononi mwake. Pumzi na uhai tunapewa bure, ndugu yangu. Jambo muhimu sana la kumshukuru huu Yesu alie jitoa akaja apa duniani ili mimi na wewe tupate ishi! Isinge yeye, ndugu yangu, hata kama unadini tofauti na kikristo, yakupasa umushukuru Yesu pia na umurudirie maana upo kwa ajili yake. 

Kama munavyo jua mwaka huu wa 2013, katika kazi za uimbaji mwezi huu wa kwanza mutanipata katika album hizi 

  • Himbaza Collection Vol1 by UBS Gospel -United Burundian Gospel Singers Group
  • HAKIKA by Hosanna Choir from Seattle, WA 
Niko naandaa kuondoa Album yangu mwenyewe ambao itakua ya pili baada ya "Uruwo gushimwa Album from 2009". Mengi zaidi nitawaelezea niko katika maandalizi kali. Hakikisheni mumenunua wadau kazi hizo za UBS Gospel na Hossana Choir, tusaidiane kuinua kazi ya Mungu. 

Heri mwaka Mpya, Heri siku kuu Njema kwenu wadau 
The Superlative Kaburungu 

Monday, December 24, 2012

Album "Hakika" Trailer ya Hossana choir

Ndugu wadau, napenda kuwajulisha yakwamba album ya Hosanna Choir "HAKIKA" ambao mulikua munasubiri mda mlefu sasa imewafikia. Album itaondolewa mwezi wa kwanza mwaka wa 2013. Katika album hiyo mutakua muna nisikia kwa masauti kwa video itakua chache kidogo kwasababu nikupata mda wa kutosha.  

Hakikisheni tumenunua Original, na munisaidie kuwakanya wale wote wanao fanya fake DVD, maana sheria itafuata mkondo wake, usiseme si kuonywa. Tayarisheni meza chakula kiko njiani! 


Tuesday, December 11, 2012

Camera Mpya

Ndugu wadau, hii ni Camera Mpya nimenunua. Mwanzoni nahisi mulikua munaniona na Panasonic Cameras, kweli nilikua big fan wa panasonic, lakini baada ya kukutana na Canon EOS au 7D, kweli nimevutiwa. Kwa picha nakuhakikishia kwamba ni Full HD; Kwa Video ndo usiseme, Video zangu zote zitakao tengenezwa na Afro Shemeza Studios, zitakua zinatambulishwa kama "Burundian Gospel Videos". Kama unahitaji uhariri wa hari ya Juu, na Video yako kua yenye kumelemeta, Compuni yangu ndo ya kutumia. Niko Available ikiwa, ni Sherehe ya harusi, Chama cha siku yakuzaliwa, ikiwa ni Video yote ile unataka, karibu. Ila kwa zaidi nitakua nachukua video ya nyimbo za Injili ao filamu za Injili. Nina Lenses mbili, yani hata kama uko mbali naweza kukukogota. Kama nilivyo waambia wadau, kampuni yangu niko naipamba moto, nikishirikiana na Kaka yangu "Silas Manirakiza"  
Tukikutana utarajie kuona Camera yangu kama hivi. Niko nanunua vifaa vingine vinge vya kupamba camera ili muonekano uje kabisa wenye aina yake. Kweli mtaona yakwamba, mimi si mtu wa kusema bila matendo na katika jamii nawaletea kitu kipya chenye maana, na katika ujio wa uimbaji wangu, nisiseme mengi mumeshaona kazi nayo fanya kwa bidii ili kazi zangu zisambalike. Haya ndugu mdau, kampuni ni yako "Afro Shemeza Studios" kuitumiaa. 

Niko najiandaa kununua vifaa vingine, kila kifaa nitakua nanunua, nitawaonyesha, maana ninyi mna nafasi kubwa sana katika maendeleo yangu, pia nawapenda sana katika Jina lake Mwokozi wetu Yesu. Nikikawiya kua blog, basi mujue kwamba nitakua niko busy na mambo furani, na munivumiliye ila musichoke kunitembelea. 

Usisahau kutembelea Official Site yangu kwa www.kaburungu.com 


Truly Yours,  
 The Superlative Kaburungu 

Wednesday, December 5, 2012

Shukrani kwa Radio Isanganiro

Ndugu wadau woooote nawasalimu katika Jina la Yesu. I jumatano tarehe 05, mwezi wa 12, mwaka wa 2012 Kijana wenu munao amini "The Superlative Kaburungu" nilikua Live kwenye radio ya Isanganiro kama nilivyo waeleza kwa facebook. Katika kipindi hicho nilikua pamoja na waimbaji maarufu apa USA na Canada, kama Witness M. Kabura, Bukuru Celestin, Abel Nkurunziza, Methusela Nzisabira, Aline D. Vyuka, Eliphaz Ntunzwenayo. Awo wote tulikua pamoja kwa kipindi hicho "Jumatano Msanii" na Mtangazaji maarufu nchini Burundi "Ernest Pablo Baryuwabo"; ndani ya kipindi tulikua tunawaakirisha album yenu "Himbaza Collection" Mwaka huu, The Superlative silali wala hakuna kuregea, niliwaaidi wadau wangu yakwamba nitawaletea Entertainment katika tasnia nyimbo za Injili, ivi sasa safari imeanza. Tutakua tena kwenye kipindi ijuma tatu (Monday) tarehe 10 mwezi huu wa 12, mwaka wa 2012. Nitawakumbusha kwenye facebook mda ukikaribia. Napenda kumshukuru sana "Ernest Pablo Baryuwabo (Mtangazaji maarufu nchini Burundi kupitia radio ISANGANIRO)" anaye nisaidia sana kwa kutangaza na kusambaza kazi zangu, Namtakia baraka kutoka kwa Mungu! hata na watangazaji wengine kama GLM & Rema FM, Mungu awape baraka kutoka kwa Mungu. Shukrani zangu pia kwa wadau wangu wote, kama si ninyi jina langu haina faida katika jamii, lakini munanisaidia sana katika kimawazo na ku support kazi zangu, Endeleeni na Mungu atawazidishia baraka, ninyi muhimu sana katika kazi hizi.


Cover yenyewe ya "Himba Collection Vol1" ni hii. Umoja katika jamii ni nguvu tena hujenga! Hawa wote niwasanii munao amini katika tasnia ya nyimbo za Injili; Album inaenda kuondolewa karibuni mwezi wa kwanza mwaka wa 2013. Usikose kuinunua CD hii maana kazi ilomwo imebalikiwa, yani imepakwa mafuta, ndugu wadau nawa amini sana kwa support mnao nipa, naamini pia yakua kila mtu apata nakala yake harisi (Original Copy). Nitawajulisha ikifika madukani..... Tembelea www.burundiangospel.com kwa mengi zaidi! 

Shukrani kubwa sana kwa Mungu anae nipa vipaji hivi, na mafanikio katika kazi zangu zote! Wadau mukiona naimba, nahubiri, nakua maarufu katika kazi zangu, ao nafanya jambo lote lile, nikwasababu ya neno la Mungu, yanu huu Yesu ana umuhimu katika maisha yangu; hivi vyote ni yeye katenda maana yundani mwangu! Heshima na Utukufu pamoja na Sifa zote vimurudilie Mungu daima yote milele! 

-The Superlative Kaburungu-