Wednesday, December 26, 2012

Heri siku kuu njema kwa wadau wote!

Ndugu wadau, nawasalimu katika Jina lake Mwokozi wetu Yesu. Napenda nitangulie kumpa Shukrani za thati Mungu anaye tuwezesha katika maisha yetu ili tuweze kufika mahali tulipo. Kama navyo pendelea kusema yakwamba, Hivi nilivyo mimi kwa leo, nikwaajili yake Yesu, kama nina vipaji mbalimbali, nasikika ulimwenguni, si mimi bali ni Yesu ndani mwangu anaye tenda kazi na ni yeye mwenyewe anaye yafanya yote, mimi sina ujanja wote ule! Utukufu, Heshima, Shukrani na Sifa vimurudilie yeye "Yesu". 

Katika kumalizia mwaka huu, Namwomba Mungu anipe nguvu na vipaji mbalimbali katika mwaka mpya ambao tunaenda kuanza wa 2013. Mwaka wa 2012 kweli nimeona mkono wa Bwana na ulikua mwaka wa mibala nyingi sana katika maisha, sikua kua kama nilvyo ao kutenda kama nilivyo tena. Namshukuru Mungu ameniwezesha nikafanya mkutano wa Vijana (CAG Ministry Youth Conference) kwahiyo Mungu apewe sifa kwa jinsi ametuezesha na si hayo tu katika mwaka huu kweli ametenda mengi, kuanzisha kampuni mbalimbali kama BurundianGospel Entertainment.  Na kundi ambalo limekuja kwa muvutio kali "UBS Gospel -Himbaza Collection Vol1-" kweli Mungu ni wa ajabu jinsi anavyo tenda kazi zake. Ndugu wadau, Mungu tukimpa nafasi ili atende ndani yetu kweli atatenda na sisi tutalizika. Tatizo hatuna mafanikio, hatuitaji kumpa nafasi pia na kumuheshimu. Maana Mungu hukaa katika Heshima na Sifa. Kinyume na hayo, Mungu hutomuona kabisa. Kumshemu ni kumusikia na kutengana na dhambi maana unajua yakwamba anayachukia hayo. Na katika Sifa, kumbuka kumshukuru maana yeye ndo anatenda, sisi ni vyombo tu.  

Basi kwa mwaka huu wa 2013, labda nisitaje eti nitafanya nini kwasababu nangojea matenda ya Bwana. Kuna ahadi zake njema tena nyingi kabisa na hizo zote mwaka wa 2013, mutaziona endapo tuaendelea kuombeana ili ule mwovu asije akajitokeza kwa majaribu yake. Nawatakia siku kuu njema, Mungu awazidishie balaka, tumalize mwaka salama na tuanze mwaka mpya kwa usalama pia. Kikubwa zaidi, tukumbuka kumshukuru mwenyezi Mungu alie tutendea ili tufike mahali tulipo, maana sisi binadamu hatuna ujanja, hesabu ya siku zetu za kuishi zimo mikononi mwake. Pumzi na uhai tunapewa bure, ndugu yangu. Jambo muhimu sana la kumshukuru huu Yesu alie jitoa akaja apa duniani ili mimi na wewe tupate ishi! Isinge yeye, ndugu yangu, hata kama unadini tofauti na kikristo, yakupasa umushukuru Yesu pia na umurudirie maana upo kwa ajili yake. 

Kama munavyo jua mwaka huu wa 2013, katika kazi za uimbaji mwezi huu wa kwanza mutanipata katika album hizi 

  • Himbaza Collection Vol1 by UBS Gospel -United Burundian Gospel Singers Group
  • HAKIKA by Hosanna Choir from Seattle, WA 
Niko naandaa kuondoa Album yangu mwenyewe ambao itakua ya pili baada ya "Uruwo gushimwa Album from 2009". Mengi zaidi nitawaelezea niko katika maandalizi kali. Hakikisheni mumenunua wadau kazi hizo za UBS Gospel na Hossana Choir, tusaidiane kuinua kazi ya Mungu. 

Heri mwaka Mpya, Heri siku kuu Njema kwenu wadau 
The Superlative Kaburungu 

No comments:

Post a Comment