Tuesday, December 27, 2011

Kazi naendelea na maendeleo zaidi

kwa kifupi ndugu wadau ni kwamba kweli muda kitambo sipatikani kwenye blog hii ila nikwasababub nilikua nimepatwa namajukumu furani na mengi hivi ya kuwaletea habari njema.


Ndugu wadau ni kwamba mimi wengi nasikia kua wananijua kama Director na nikweli mimi ni Director wala sitabadilika kamwe ila bado naendelea zaidi ya zaidi. Ivi sasa mtakua munanipata kwenye movie za ki Kristo kutangaza injili ya Mungu zaidi kutumia kuhubiri na mambo yama filamu kama munavyo jua wengi kua filamu ni moja kali ya ushauri. Mwaka huu wa 2012 nakuja kiupya tena zaidi ya zaidi kama vile Mungu alivyo agiza na ametimiza. Basi ndugu wadau tuendeshe kazi ya Mungu mbele kwa kukumbuka tulipo anguka na tumurudilie bwana. unaweza kufikiri kua nimeokolea kwa sasa, sikusema ivo ila nikwamba tangu mwanzoni nilikua mkristo ila nilikua na kimbia sana na maisha ya dunia angalau nipate maendeleo ila nigunduwa ni wapi mafanikio anapatikana, ni kwa Mungu kabisa na kwa hivi naendelea sana kwa bidii...


Mwaka wa 2012, Kijana wangu ''Johnson Mkubwa'' anakuja na filamu inaitwa ''Get saved to be Blessed'' chakula ni chenu nitawaeleza ni lini itaondolea maana movie hiyo itafanyiwa kazi (uhariri) na kampuni yangu (Afro Shemeza Studios/Store). kuweni hewani na kutembelea sana blog yangu bila kusahau kampuni yangu ingine ambao inatangaza filamu hizo ''Ugleawood Entertainment''(ugleaworld.ning.com)


Kwa zaidi mwaka huu wa 2012, mutakua munanisikia sana kwa mahubiri ya Mungu na kwa kifupi tuna mkutano wa Vijana July 7-8, 2012 in Dallas, TX  unakaribishwa ndungu mdau kwa kupata balaka kutoka kwa Mungu maana Mungu ameyaanda mengi kwa watu wake! Mengi zaidi mutayajua kwa kufuatia blog yangu na nitapenda sana maoni yenu kwa ku comments hasasa kwenye Ugleaworld.ning.com ili tuendeze kazi mbele!


Karibuni kwa ''The Superlative Kaburungu'' kizazi kipya na ''Maendeleo kali''

Friday, April 29, 2011

21Days Ipo madukani sasa. Pateni nakala zenu...


Basi ndugu watazamaji hatimae 21Days yaingia sokoni. wadau wangi walikua wakinipigia simu na kunitumia messages wakidai ni lini movie itaondolewa, nami nilikua nawajibu kua bado kweli filamu ingali inahaririwa na kuchunguza kama kweli tutaondowa kitu bora. tulikua tunahakikisha ila filamu iwafikie ikiwa bora. basi japo imechukua mda kidogo filamu kwa sasa ni yenu, jipatie original copies.  

Tuesday, March 15, 2011

Movie yenyewe ni hiyo


Hii ni front cover ya 21Days movie. wadau na mashabiki naweza tangulia shukurani kwa Mungu, naimani filamu itawafurahisha japo kuna mabadiliko kidogo yametokea. katika shooting, kikosi cha B-Squad kutoka New York walitutembelea kwa kusaidiana na ku support. Filamu imeshafika ndani ya Afro Shemeza Studios kwa uhariri muda sio mlefu mzigo unaondelewa. basi kaeni makini mujitayarishe mezani kwani chakula kinakaribia kuwafikia na mutaniambia wenyewe. 

Johnson Mukubwa kwa mala ya kwanza yeye kucheza filamu, anasema hakutegemea angefanya alivyo onyesha katika filamu hiyo. Mwana dada Irene Kasongo (in cover), naye kafumua zake na kuwapa burudani ya kweli bila utani. 

Friday, March 11, 2011

21Days inavuma ngoma

Wadau 21Days inakaribia kuingia studio kwa uhariri, The Superlative nikawa naitendea haki. apa nikawa na shoot moja scene katika filamu hii.

Uyu ni mama Kamikazi katika moja ya scene in movie, akawa anapata maelezo ya kufanya. Mama huyu ameonyesha uwezo yani apa atawapa burudani. sipendi nimusifii kwa sasa ngojeeni mzigo utoke mutaniambia.

Mwana dada  Yvonne Ndayisenga ''Shenaiza'' ameingia katika tasnia ya UGLEAWOOD Movies, hapa akiwa tayari ku shoot movie. subirini awape zake huo mwana dada. 

Wadau huu ni Johnson Mukubwa anasema kua anaenda kua bega na mimi mpaka anawaonyesha uwezo wake, yani kwanzia leo ni swahiba wangu. ndipo akapenda ni mupe nafasi ya kuonyesha uwezo wake yani apo ametoka Canada mpaka USA. wadau nimependa uigizaji wake hadi mwenyewe sikutegemea kua angefanya nilio yaona. kueni hewani mzigo unakaribia kuondolewa. 


Wednesday, March 9, 2011

Ndugu wadau nakaribia kuapa mzigo wenu, mimi hapa nikiwa katika maandalizi

Wadau na wapendwa wote kama nilivyo wa aidi kama nitakua nawa blog na kuaeleza kazi zangu, basi huu ni mimi mwenyewe The Superlative nikiwa Boston, MA ndani ya Mall apo mchezaji wangu mpya Nyandwi zebedayo ''Robot'' akawa amenipeleka mitaa mbali mbali kwa maongezi zaidi ya filamu. Kijana huu anachekesha, kwa maongezi yake utakutwa umesha sahau na kile ulicho kipanga kufanya na amenihakikishia kua anaenda kuonyesha uwezo wake hasasa baada ya filamu hii.  

Apa ni mimi na mchezaji mpya Nyandwi Zebedayo ''Robot'' (left-kushoto) yani baada ya maongezi tukaon vizuri twelekee nyumbani ndipo sasa kidogo tukachukua ma pozi. 

Ndugu wadau mzigo huu unaenda kuwapa burudani na sipendi nijisifie ao nisifie filamu kabla hijaondelewa, wenyewe mtaniambia mzigo ukisha kua mitaani. kaeni kwamakini nitawapa Surprise week hii.


Wednesday, February 23, 2011

21Days inakalibia muda sio mrefu...


Napenda kutangulia kuaomba radhi siku nyingi sipatikani kwa blog hii, nilikua bado na burudika na mapumuziko pia na kazi zingine ila naona mapumuziko yameisha narudia kazini rasimi na muda sio mlefu movie murikuwa munangojea muda mrefu sana basi itaondolewa mwezi huu wa tatu (March). 


Basi mutajiuliza mengi kuhusu movie hii 21Days kwanini commercial ya kwanza na cover images haiko kama leo? ki ukweli wadau,  nilipenda niwape burudani ambao itawahakikishia kua mwenyewe The Superlative kazi naiweza na sio muchezo. nimeibadilisha kabisa iko mupya na tena kwenye kiwango cha hari ya juu.  naimani wadau wengi hapa USA & Canada mutaipenda sana. wechezaji ni wapya sijawai kuwatumia ila jinsi navyo waona kuweni tayari kuwapa ufunuo wa filamu. siwezi wasifia kwa sasa, napenda muitazame kisha wenyewe mutaniambia. 


Ndani ya siku chache nitawaonyesha Cover mypa ya Movie hii, na Movie Trailer. 
Kueni makini nimerudi apa blog nitakua nawajulisha kinacho endelea. 


Bado inatayalishwa na Afro Shemeza Studios (UGLEAWOOD Movies, www.ugleaworld.ning.com)



Tuesday, February 1, 2011

''Uruwo Gushimwa'' Album


Hello fans, Just reminding you about my First Album ''Uruwo Gushimwa'' which gives me a honor to pray or worship the Lord. Thanks to those who give me congrats for it and I really do appreciate it a lot. 

So if you haven't listened to it take a chance to visit my Youtube Channel at www.youtube.com/vyamungu25 or win a free CD when 21Days comes out.