Friday, October 12, 2012

Fursa ya Methusela Nzisabira

Ndugu wadau huu ni kijana anaenda kwa Jina "Methusela Nzisabira" ndo majina yake kamili. Kijana huu ni mufanya miziki za nyimbo ya Injiri, anaishi apo Dallas, TX. 

Katika safari yangu ya kwanza kwenda Dallas, Texas kwa ajili ya mkutano wa Vijana (CAG Ministry Youth Conference) ulio fanyika mwezi wa 7 tarehe 7 na 8 mwaka wa 2012, na katika maandalizi ya mkutano huo, kijana huu alinisaidia kwa mambo mengi sana. Na cha zaidi na mushukuru kwasababu alinikabizia Van (gari) yake, kwa hizo siku ambazo nilikua naishi apo Dallas. Munajua ukiwa mgeni ni vigumu sana kuhusu usafiri na nirikua sina uwezo kabisa wa kukodisha (rent) gali, ila Kijana huu kajitolea ili niitumie gali (White Van) yake, namshukuru pia kwa Heshima alio nionyesha na ukaribisho wake kwa kunipokea kama mtumishi wa Mungu bila zalau wala nini, ingawa wote ni Vijana unakuta kuna maongezi furani yanamuchukiza Mungu, ila Bwana asifiwe maana kazisahau dhambi na makosa yetu. Namuombea balaka Kijana Huu Mungu amuzidishie Hekima na busara katika kazi zake zote na akumbuke kumuheshimu Mungu na kuendeya njia za Bwana kila kukichapo. 

Kwa kifupi ndungu wadau, Napenda kuwatangazia ya kwamba, kama unataka kufanya kazi yako nzuri ya audio production (kurikodi sauti), nakushauri umukabiziye kazi zako Kijana huu, maana alinionyesha uwezo wake, na katika Studio yake niliingia, nikaitembelea hata kulikodi nimerikodi nyimbo mbili ambazo nitaziweka katika album yangu ya pili. Katika miziki hiyo kijana amenisaidia kurikodi na kupiga vyombo kama Electronic Keyboard (piano), Gita (solo).  Yani hatakurikodia tu masauti, na katika mziki wa kweri nakuhakikishia kua ataweza na wewe utapenda kweli. 


Hii ni moja kati ya zile nyimbo mbili nimerikodi katika Studio yake. Mausauti ni mimi The Superlative mwenyewe, na vyombo: Base (mimi), Keyboard (mimi na Methsula, ila mimi nimecheza kasauti ambapo kanasikika kama Violin or whistle, mengine ni Methusela)  


 Hawa ni warembo katika kundi (Choir) lililotoka Abilene, TX kwenda Dallas, TX kurikodi ndani ya Studio hiyo la Methusela, inaitwa "GAP Studios -Glory Ambassadors Pro" Ivyo basi kaeni tayari Album hiyo inakaribia kuafikia endapo makandamizi yakimalikiza. 


Nafikiri mnamuona na yeye kwenye mtambo ya mziki akiwa na gita (amevaa rangi ya blue, In blue behind the guy in red) 


Kama kawa akiendelea. Kijana anaejiita "Dr. Pastor Eric" mtunzi (Owner and Operator) wa website ya www.africamusicproduction.com, uwo kwenye upande wa kushoto akikaa amejishangaza sijui kashangaa nini! hata na yeye alikuwepo akisikiliza makatandamizi ya kwaya hiyo. Na wanakwaya naona wakapa mapozi kidogo, ao sio. 

Basi nitajitaidi niwajurishe mkanda (CD) ikiondolewa ili nanyi mujipatie raha. Tafadhari tuwe tunasaidiana Jamani. Wenzetu wakifanya mambo, basi tununue ili tupate kuendelea mbele, na tuhakikisheni tumenunua Original Copy. 

Tuesday, October 9, 2012

Je ni kweli Maisha yanachanganya?

Sababu yakulinga, tumwo ndani ya Yesu, sikiliza tafandari usipuuzie. Naomba pia ukisoma apo chini uwezi ku Comment, ili umubaliki mwenzako atakae soma hii. Unaweza hata kuongeza maoni yako, utabalikiwa kwa maana utakua umewasaidia na kuwafurahisha wengi wanao sona Ujumbe kutoka blog yangu hii. Asanteni! Haya, tusome sasa, ...


Ndugu zangu katika Jina la Yesu, hua kuna swali Vijana wengi tunapendelea kuuliza ao kusema. Je Maisha yanachanganya? Vijana wengi wanadai yakwamba maisha yanawachanganya ndo maana wanaangaika uku na kule ili wapate maisha. Wengi hukimbilia katika usanii kuimba nyimbo za kisanii, na wengine hukimbilia katika sanaa (movies), wengine wanadhiriki hadi kufanya kazi mbili au tatu eti apate maisha bora, na hapo kanisani haudhurii. Unakuta na wengine wanaendea njia nyingi eti mladi wapate maisha. 

Nisikilizeni enyi wote vizazi vya Mungu, Maisha hayachanganyi ila sisi ndo tunayachanganya na kujichanganya wenyewe. Unakimbilia kuimba nyimbo za kisanii, unamsifu mwana mke ao mwana mme badala ya kumusifu Mungu. Na katika huduma hiyo, Vijana, nawatangazia yakwamba hakuna mafanikio hata siku moja. Ni hakiri gani kumsifu mwana mke ao mwana mme ambae ni mavumbi kama binadamu wengine? Kisha faida gani utakao itoa kutoka katika huduma hiyo ya kumusifu? malipo gani umepata kutoka kwake? Hamna, tena haitowai kutokea mwanadamu kurizisha moyo wako hata siku Moja. Pia mnajua yakwamba, "amelaaniwa amtegemeae mwanadamu" ndivyo munavyo Jiletea laana na mikosi katika huduma hizo, baadaye mnalalamika eti maisha yametuchanganya, tunajaribu kuyatafuta huku na kule. Maandiko katika kitabu cha mwanzo (Genesis 1:28-29) yanatwaambia yakwamba baada Mungu kuumba mbingu na Nchi akamwumba mwanadamu, alisema pale mstari wa 28, zaeni mujaze ulimwengu wote, nawapa kumiliki vyote vilivyomo ulimwenguni. Na hayaishii hapo tu, baada ya pigo kali wanadamu walio pata enzi zile za Nuhu, Bwana alimwambia Nuhu na kumwaidi vile vile kua hatoangamiza tena binadamu kwa maji, na akamwambia kua watamiliki wanyama na vyote vilivyomo ulimwenguni (Genesis 9: 1-3). na tukumbuke sote tulizaliwa baada ya hao. ] Kama Mungu alisema hivyo, waweza kusemaje yakwamba maisha yamekuchanganya? Mungu alie kuumba anazo sababu za kukuumba wewe pia anayo huduma yakutosha ili akutunze. Kama angeshindwa kukutunza hange kuumba, ungekua umefariki kama wale watoto wadogo wanao fariki wakiwa wachanga sana ao hata kuzaliwa hungezaliwa. Ila kwasababu ameona kua anao uwezo wa kukutunza ndo maana akakuacha ukakua Ila umekua na ukabadilika. Nilikupanda uwe muzabibubu mwema, umegeukaje kua mzabibu mwitu? Bwana kasema (Jeremiah 2:21)! Tukiendelea pia kusoma maandiko matakatifu katika kitabu cha Jeremiah 4:18 panasema yakwamba "Njia zako na matendo yako ndo yamesababishia hayo (magonjwa, mkosi, mapigo, shida, etc), huu ndo malipo ya uovu wako. Ni kweli ni uchungu tena yanafikia hata moyoni mwako)."Tukiendelea kidogo kwenye msitari wa 22, Bwana alisema: "Watoto wangu ni wa pumbavu, hawanijui wala hawajui njia zangu. Wana hekima ya kutenda maovu ila hekima ya kutenda mazuri hawana." Jiulize sasa mwenzangu, bado walalamika eti Maisha yanakuchanganya? Ebu tusilikilize maneno Yesu alio sema katika kitabu cha Yohana 8:12 akiwa anaongea na wafarisayo, akasema: "Mimi ni nuru ya ulimwengu, na yeyote atakae nifuata, hataona giza kamwe (Giza inahesabiwa kama Magonjwa, shida, majaribu, mikosi, uhalibifu, etc). Badala ya hayo, atairidhi Nuru ya uzima wa milele." Hii inatuhakikishia yakwamba kumfuata Yesu ni kupata maisha yario bora pasipo shida na majaribu. Sasa wewe kama mkristo, kwanini unakutana na hayo? Jamani tusimulaumie Shetani, maana sisi ndo tunamtafuta badala ya yeye kututafuta. Biblia inatuweka wazi jinsi ya kujilinda na ule mwovu. maandiko yanasema katika kitabu cha Jacob 4:7 neno linatwambia "Basi mtii Mungu.Mpingeni Shetani, naye atawakimbia." ukiendelea katika mstari wa 8, panasema: "Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu enyi wenye nia mbili. Tukisogea kidogo pale kwenye msitari wa 10 panasema: "Jidhirini mbele za Bwana, naye atawakuza." Tuseme nini sasa Vijana! Unataka turudie tena kuawambia amri za Mungu. Shetani ukimukaribisha atakuendesha kweli kweli, ubaya wake anakuendesha kama gali mbovu, hujui niwapi maisha yako yanaelekea, ndo maana unahangaika. Yesu ndo mwanzo na mwisho, pia ndo funguo ya maisha. Hakuna aliye kuja kwake akaadhirika wala kupata shida. Alituaidi yeye mwenyewe katika kitabu cha Yohana 10:27-30 Yesu akasema: "Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami huwajua, nao wanifuata. nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakae wapokonya (yani kuwatoa) katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni Mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa baba yangu. Mimi na baba tu umoja." Kijana ao mtu yeyo unaye sikia maneno hayo, hivi unajiuliza nini ao unangoja nini kumpa Yesu maisha yako. Maisha hayatafutiwi katika hanasa za dunia, wala katika tamaa za myili yenu; amna kabisa, maisha ni kwa Yesu pekee, yupo tayari kukusaidia. Waweza kuniuliza; mimi sina Yesu wala mambo kama hayo, mbona naishi vizuri. Jibu: "Mambo yote ya dunia hii yatapia, ila neno lake Bwana ni uzima wa Milele" Ebwana we, hata Shetani anawasikia walio wake na kuwapa maisha ya mda kitambo tu, jiulize kwanini ameleta AntiKistro! Wewe unakaa apo eti unamwabudu Mungu, kumbe unamwabudu Shetani; hua na yeye maombi yetu anayasikia, kisha Antiskristo akifanya kazi eti Mungu kanijibu, tafadhari pima kua Jibu zote zimetoka kwa bwana (1John 4:1-6), wakristo kaeni macho. Kijana kama unavimba, vimba na Yesu; dunia hii siyakwako. Msichana kama unalinga, linga na Yesu; dunia hii siyakwako. Hata na sisi tunaweza kua wasanii tena kuazidi, ila yote tunayafanya kwa mapenzi ya Mungu. Usijivunie mali wala vipaji kaka na dada zangu, ila Jivunie Upendo na neema za Mungu tunazopewa Bure, Mungu kasema hayo katika kitabu cha Jeremiah 9:23. Ulimwengu tunapita, wote tutaozea kaburuni bali walio mfuata Yesu, hawata shududia kifo hata kidogo, maana kifo ni njia yetu yakwenda Mbinguni. tutamraki Bwana mawinguni. Malipo yote nihapa hapa duniani. Bwana ataturipia hapa duniani wema tulio ufanya, kisha taji ya uzima wa milele uko mbinguni. Kwenu nyiye mnao jifanya niwakristo kumbe amri za Bwana hazipo miongoni mwenu na ninyi wenye dhambi, malipo yenu ni hapahapa ulimwenguni kuteseka kisha baadaye kufia jehanamu kwenye moto wa milele. 

Nashangazwa sana na watoto (wasichana na wavulana) wa wachungaji. Ikiwa baba yako ni mchungaji, Mwarimu ao cheo furani kanisani, Jamani nyiye wanao mumebadilika sana. Bwana Yesu alisema pale katika kitabu cha Yohana 5:19 yakwamba hakuna chene mtoto anafanya pasipo kuiga babae, maana babae humufunza njia zote za haki." lakini vizazi vya leo badala ya kufuata tabia na nyendo za wazazi wenu (wachungaji, etc), nyie watoto wa wachungaji mumekua kelo kwa wazazi wenu. Wengi ni wasanii, wakahaba, kuvaa nguo za aibu, tabia chafu na mengi zaidi yakufanana na ndambi. Katika kitabu cha Mithali sura 30:11 panasema yakwamba: "Kuna vizazi havieshimu baba zao, na wengine hawabaliki mama zao." ndo mulivyo katika ulimwengu wa sasa. Neno la mungu linasema: "Waheshimu baba na mama ili uridhi Nchi Bwana aliye kupa, na amelaaniwa atakae tukana wazazi na kuwazalau ao kutokusikia ushauri wao." Jiangalie usije ukakute kumbe umelaaniwa zamani. Nuhu alimulaani mwanaye kwakunchungulia uchi wake, natena laana ilimushika kweli kweli (Genesis 9:18-27). Ndo maana utakua unafanya mambo na hufanikiwi, wazazi wako wanakuombea ili umurudilie Mungu, nakwambia wazi hutokwenda popote; ni mambo haya mawili: utakutana na shida kisha kifo, ao mwisho wake utamukumbuka Bwana."  Basi, kumbukeni mulipo anguka na mukatubu makosa yenu. Yesu yupo tayari kuwapokea na hatowaacha kamwe! 

Tembelea www.kaburungunews.blogspot.com na usipuuzie, pia usitazame sanamu tu ila soma maandiko na utabalikiwa. Mpeane Ujumbe huu kwa wenzenu wote mnao jua, mutabalikiwa na Mungu. 

Friday, October 5, 2012

Ikingera, wimbo katika Album natarajia kuwapa karibuni ivi

Romans 7:14-25, Hebrews 12:1

Ndugu wadau, nawasalimu wote kwa Jina La Yesu! Huu ni wimbo nilio aidi wadau wangu kua nitawatilia kwenye Youtube kabla ya kuondoa album. Nime aidi nyimbo mbili tu, ila kwanza nawatilia huu, mwingine nitatia badaye. wimbo huu nimeurikodi katika studio ya Methusela Nzisabira (GAP Studio "Glory Ambassadors Pro Studio") mjini Dallas, Tx. Baada ya mkutano mwezi wa 7 mwaka huu wa 2012 nikaona nitembelee studio ya Kijana huu kama mrundi mwenzetu na tangu apo tukawa marafiki na kuanza kuongea mengi kuhusu utengenezaji wa Audio. Vyombo katika wimbo huu vilipigwa na mimi pamoja na Methusela nzisabira, masauti yote ni mimi mwenyewe Kaburungu. sirikilizeni na mujifunze. 

Utumwa katika wimbo huu nikwamba mala tunakutana na majaribu mengi na mambo yanao tuzuwia kuifanya kazi ya Mungu, kama facebook, simu, Internet. Wakristo unakuta tunatumia mda wote wetu kwa mambo hayo badala ya kusoma biblia na kuomba, kufunga (maombi) na kumuheshimu Mungu. Kile tunacho taka kufanya sicho tunacho fanya. Tamaa za mwili zimetuteka. Wengi tulibadilisha maumbile yetu, wengine tunavaa nguo zisizo pendeza (aibu mwanamke kuvaa suruwali, nguo kama mini, hereni na mengeneo hivi ya kufanana), wengi tunadai yakwamba Mungu anaangalia moyo pekee ila anaangalia vyote ( Ezekiel 44:9) kuingia katika ufalme wa mbigu ni razima uwe safi mwilini na moyoni. Si hayo tu, kuna ukahaba, uzinzi, uongo, umbea, ujambazi, mambo ya kisani, na mengi ya kufanana na dhambi. Ni bora tujiepushe nayo maana tumesha tekwa na minyororo ya shetani kama vile anatuendesha kama gali mbovu. ni vizuri tujiangalie mambo tunayo yatenda tusije tukajikuta ni watumwa wa shetani. Wewe kuimba, kuhubiri, kufanya kazi furani ya Mungu haikufanyi kua uko msafi, kama bado una tendo la kufanana na ndambi bado wewe ni mtumwa wa shetani. Tumefungwa na tamaa za mwili ndio maana hatuwezi kuona ni wapi tunaelekea pasipo kufungua macho ya kiroho tujue ni wapi tumekosea na tumurudilie Bwana. Mafanikio na mazuri yatakua mbele zetu ila matendo yetu mabaya ndo yanatusababishia mikosi, magonjwa, laana, shida mbalimbali (Jeremiah 4:18); ndo malipo ya ubaya wetu. utavuna ulicho panda ndugu yangu. Tutambue na Shetani (kutumia Antikisto) anafanya miujiza, si kila jibu lote limetoka kwa Mungu, tafadhari jaribu kwanza ukajue jibu limetoka wapi. Unapo omba shetani huwa anasikia maombi yako, badala ya Mungu kukujibu shetani atajipendekeza ili aweze kupata njia ya kukuharibu. Ndo badaye sasa utaanza kulalamika eti kwanini Mungu amenijibu na ikaharibika ao ikageuka kua kikwazo? Mungu akijibu anajibu wala hakuna mabadiliko, tukimtii na kuziendea njia zake zote za haki, mkono wake utakua nasi milele daima. Ni vyema sasa ujichunguze vizuri mala kwa mala ili uhakikishe kabisa unatembea katika mapenzi ya Mungu. 

Burudikeni na wimbo huu, pia muniombee ili Album nije niitoe salama. Kama unataka kusaidia, msaada pia unaitajika. Ikiwa ni kwa maombi ao kwa kila kitu chochote kile, kikitokea moyoni mwako, Tuatabalikiwa wote. Tusisikilize tu bila kujifunza, bali tusikie na tujifunze, maana Yesu alisema heri anaye sikia na kutenda (Kusikiriza na kutenda). Tuambiane pia tushauriane wote, kama umefanikiwa kusikia wimbo huu, basi utangazie kwa majirani na ndungu na Jamaa utabalikiwa, maana utakua unaitangaza Injiri ya Bwana kama vile alivyo sema; "Enendeni Muyageuze mataifa yote kua wanafunzi wangu! mujuwe hili: nipo pamoja nanyi siku zote, hadi siku za mwisho" Yesu kasema! 

Mbalikiwe 
The Superlative Kaburungu  

Wimbo ulio changanya wadau wengi

Ndugu wadau na mashabiki, marafiki na jamaa, hii ni wimbo nilio imba mwaka wa 2010 nikiwa katika mjini Seattle, WA baada ya kuondowa Album yangu ya kwanza "Uruwo Gushimwa" mwaka wa 2009. Basi nikataka kuifanya Album ingine ya pili nikaandaa wimbo huu ila Mungu akaniita nifanye kazi furani ya uhubiri na mambo mengineo. Rakini hata ivyo nimepewa neema kutoka kwa bwana niko natengeneza Album mpya "Music Video" karibuni mwaka wa 2013, kwa sababu naisubiria Album nilio tengeneza na Kwaya Hossana apo Seattle, WA iondolewe. 

Wadau wengi hua wanasema hii nyimbo ni ya mapenzi, labda kwasababu mwendo wa nyimbo unafanana na Hip Hop ao kama nyimbo za kisani. Kipaji nilicho nacho naweza kuimba katika Style yote ile ingawa si style zote ila nimefanikiwa kuimba katika style nyingi. Hii wimbo si ya mapenzi ila ni ya kushauri Jamii: "urukundo nagukunze ngo tubane amahoro, ariko ukampora uwo ndiwe, ubwoko nakaranga." Katika jamii zetu za kisasa watu huzarauwana ao kuchukiana kutokana na ukabira wa mtu ila sisi wote tumeumbwa na Mungu mja. uwe muisilamu, uwe mukristo, uwe na dini gani ao kabira ipi, ujuwe yakwamba sote tumeumbwa na Mungu mmoja alie hai, Muumba wa mbingu na Inchi maana Dunia na vilivyomo ni mali ya bwana. Tupendane, tusichukiane, kama Nchi zetu za Africa, tuwe na umoja katika maendeleo ya kimaisha. tusibaguwane wala tutengene, tujue upendo wa Mungu jinsi alivyo tupenda bila upendeleo, anamwinua anaye mtaka na anamushusha anaye mtaka. Mawazo yake na njia zake sikama za mwanadamu. Basi tufuate mtindo huo wa Yesu. 

Naimani tumeelewa ya kwamba wimbo huu si wa mapenzi ao nini, ila ni ushauri kwa Jamii zetu. Walio kua na maswali na Imani mmelizika na nawashukuru kwa support yenu na maombi yenu ili kazi ya Mungu iendelee, tuendelee kupendana hadi mwisho wadunia. 

Mungu awape balaka na Hekima
The Superlative Kaburungu 

Monday, October 1, 2012

Wa dada zetu warundi walituaga duniani

Wa dada wenzetu "Vestina & Violette" walikua wana ishi mjini Amarillo, Texas. Wasichana hawa walikua na umri mdogo kama 11 ao 12-13, waliiaga dunia tarehe 30 mwezi wa 9 mwaka huu wa 2012 masaha ya jioni kuanzi kama sa 8pm.  

Habari zina twambia yakwamba waliuwawa baada ya hajari, tena alie wagonga hakusimama aliendelea kuitembeza gali bila kuwajari. Baada ya kugongwa wasichana hao walisimama na kumbea ili watoke balabalani, cha kushangaza na kuuma nikwamba walipo vuka balabalani wakauwawa. Mmoja aliuwawa aipo fika kwenye ukuta ao uzio (Fence, kirundi: urupango) kwa wajirani, mwengine akaja kuuwawa polini (nahisi alikua njiani akielekea nyumbani) 

Kinacho nisikitisha, hawa madogo zetu (wasichana) katika kutembea kwao walikua wanatokea kusukwa meshi na mama mmoja hivi kama jirani yao. Sasa ndipo walipokua wanaelekea nyumbani wakapatwa na hajari hiyo. 

Nataka nitoe mashauri kidogo wa dada zetu tulio fanikiwa kupata pumzi leo na tumushukuru Mungu kwa hilo. Dada zetu, naomba tuisikie sauti yabwana tunapo shauriwa, nikwamba tulifika huku malekani, tukaanza kubadilisha mwili yetu, wengine kugeuza nywere na mengi zaidi furani. Jamani Bwana alisema kua tukifika katika nchi hizi na kujigeuza kiukweli tutashuhudia mkono wake na tutahukumiwa. usingojee eti kutakuwa na mwisho wa dunia ndo tunyakuliwe; Bwana wetu Yesu alisema, palipo wawili patanyakuliwa mmoja, na palipo watatu ao ine, tano, sita kuendelea, patanyakuliwa wachache wengine wabaki. Ukiona nalia kanisani usinishangae, nawalilia ndungu zangu, walio fungwa na dawa za kurevya, washerati, waongo, wazinzi, makahaba, majambazi, wauwaji, na mengineo yakufanana na dhambi, ili waokoke. Nawalilia pia ndungu zetu walio fika uku malekani wakaa kubadilisha myili yao kua byashara, wengine wakasuka meshi, wanawake kuvaa ma suluwali na hereni na mengineo zaidi ya kuchafua mwili yao. Je hatujui yakwamba mwili yetu ni hekaru la loho mtakatifu? Hata na wanaume wengine wamefuatia mtendo huo wakuvaa hereni na wengine kuvaa nguo zao kinyume na heshima kama mkristo ao kama mwanadamu alie umbwa na Mungu. Tafakarini siku tunazo nichache sana, Hujui ni lini siku yako. tumewakosa dada zetu "Vestine and Violette" Je ninani anajua Mwisho wao? Mungu pekee. Kinacho nisikitisha waliuwawa na meshi kichwani, na alie wasuka meshi hizo hua na yeye damu zao zitamfuata. Heri amrudilie Bwana mapema atubu dhambi zake, na si vyema kuasuka meshi wengine maana unaunga mkono mwovu shetani pia unasababisha wengine kuyaona mapigo ya Bwana. Bora kuwashauri  na kuwafundisha njia za Bwana badala ya kuwasuka. Jiulize mwenzangu, ukifa leo, utakuwa mgeni wanani? mambo unayo yatenda mwenyewe unajua, Je utapokelewa na wanani? Mashetani ao malaika za Bwana? Jiangalie katika nyenendo na matendo maana mwisho tumesha ufikia usingojee eti unakaribia, na sisi tunaelekea huko, Swali kwako; Je utakua mgeni wa nani? Sisi tulio ukoka tutakua wageni wa Yesu, mkubali yesu kua Bwana na Mwokozi wa maisha yako akusemehe dhambi ulizozitenda. Kifo hakijari umri wala masomo wala uzuri wako, kifo wala hakitajwi eti sijaowa sina watoto, kifo hakina huruma. Shetani anazunguka kuzitafuta roho zawatu nawaoneya huruma mnao mkataa yesu. 


Vifo vya kujitukiza duniani Vime enea, Jana alikua mzima leo tunaambiwa kafa. Ukimwona kwenye jeneza, utazani ataamka , mtu na hafya yake kaburini anakwenda. Ndugu zangu ni heri tutengane na Dhambi tumrudilie bwana mapema, yuwaja mawinguni, leo ni hawa dada zetu kesho ni sisi, Je tutapokelewa na nani? 


Mungu uzilaze mahali pema peponi roho za wadada zetu "Vestine & Violette". Nawaombea balaka na faraja kutoka kwako Yesu, wazazi na ndugu na marafiki wawalio achwa na dada zetu. Acha uwitwe Mungu maana ndivyo ulivyo. Uokowe nafsi zetu pia uponye roho na mwili vyetu, sifa na utukufu vikurudie Bwana ambae unatoa na unatwaa. Nani wakukupinga? Njia zako sikama za mwanadamu, na mawazo yako si kama ya mwanadamu. Mungu uwimidiwe daima Amen. 

The Superlative Kaburungu 

Sunday, September 30, 2012

Uncle Jimmy Kaleta fursa ya kutisha katika tasnia ya Comedy & Drama

"Uncle Jimmy"
Wadau wangu wote, na Imani huu kijana wengi munamjua katika movie nilio mshirikisha ya 21Days. Kwawalio nunua full original DVD ya movie hii (21days), mwishoni mumeshuhudia Comedy nilio ifanya naye kwa maongezi furani; na ndani ya movie alikuwemo maana alicheza na warembo katika scene ya Club. 

Kijana huu anaenda kwa jina la "Uncle Jimmy"Anaishi Boston, Massachussetts USA.  Katika safari (ao Experience) yakuigiza filamu, kijana huu ametangulia kwa filamu nilio mshirikisha ya 21Days ilio rikodiwa State ya Vermont. Kwa maongezi nilio kua naye, kweli nimejua yakwamba Comedy na Drama anaziweza pasipo masiara. ivi sasa baada ya hayo, amekuja na filamu ya Comedy ambae inaitwa "Crazy family" Na katika kuongea na kaka yake "Felix", nikwamba apo Boston, MA kuna kikosi kali kinatengeza ma filamu; karibu firamu tatu wamesha tengeneza ila bado hazijaondelewa kutokana na kuwaandalia uhariri wa hari ya Juu kwamba watowe mzigo ulio bora. Na katika ma filamu haya mtakutana na Uncle Jimmy kuaburudisha Comedy na Drama zisizo kifani. 

Ebu mwenyewe Jionee Trailer ya "Crazy Family". Bonyeza apa 
Na kwenye Youtube Channel yake inaenda kwajina "Nyandwi Augistine" utashuhudia video zingine zake maana hata maongezi yake mwenyewe yatakuhakikishia yakwamba, burudani ya Comedy ipo kwake. Nakusii madau zangu, malafiki na fans ya blog ao kazi zangu, musikose nakala zengu ndembo za rangi ya kumelemeta yani "Original DVD" mujipatie Burudani. 

Sikiliza alivyo fanya ndani ya 21Days Movie. utamuona kuanzia 2:13 


Kama bado hujapata nakalo yako harisi, ni mda wako sasa wakuipata, wasiliana nasi kwa mengi zaidi. 

Saturday, September 8, 2012

Aline Vyuka AKA "Vyuka" Moja Burundian Artist in the USA

Aline Vyuka AKA Vyuka “Movie Director, Editor, Actress, and Gospel Artist” Msichana huu anatesa BAHOWOOD Entertainment State ya South Dakota, pia ni Kiongozi “Funder and Director” wa BAHOWOOD, Sioux Fall, SD.


Msichana huu naimani wengi munamujua katika movie ariyo igiza “Familly Issues” wengi hapa malekani walipenda movie hityo kwasababu kuna mafundisho mengi ndani ya filamu hiyo. Vyuka pia ni Muimbaji wa nyimbo za Injili (Burundian gospel Artist” kama huja pata bahati ya kusikiriza nyimbo kutoka katika album yake ya kwanza, ni bahati yako sasa.

Sikia wimbo wake, moja kati ya Album yake "VYUKUSENGE"  


Album Trailer:


Hii nazo ni trailer ya movie ariyo tengeneza na kuigiza