Tuesday, December 24, 2013

Safari yangu ya kwaga mwaka huu wa 2013, ambapo nilikua Missouri na Colorado

Kwenye picture ni mimi (Right), na Murishi Yaya AKA Solo Kibangu (Left), Kijana huu tumekutania Kansas City Missouri, na kweli nimekubali kazi yake yakupiga guitar cha Solo. Kijana huu tulikua tunaongea kawaida kwenye simu basi ikabidi tuonane uso kwa uso, na baada ya kukutana tukagundua kumbe sisi ni familia kabisa ya ndani.

Kabla kuingia Kansas City, Missouri; nilikua Columbia, Missouri ambapo nilipakaa wiki tatu mzima. Uko nilikua katika kazi ya kutengeneza miziki (Beats) na kweli kama kawaida yangu kwa uwezo wake roho mtakatifu niliweza kuwatengenezea beats zaidi ya 40. Ninavyo vipaji vyingi sana ndani yangu na nimemuaidi Mungu kua nitavitumia vyote kwa pamoja, na nikweli Mungu yupamoja nami katika kazi zote zile.

Sikia wimbo ambao nimefunya na Kijana Murishi Yaya in Kansas City, MO
http://www.youtube.com/watch?v=ubbugPmh7Oc&feature=youtube_gdata

Wimbo haukufanyiwa Mixing kwasababu nilikua katika harakati ya kwenda Denver, Colorado

Baada ya hapo Tarehe 8 mwezi wa December 2013, nikaingia Denver, Colorado ambapo na penyewe nilikua natengeneza Beats za Kwaya furani hivi.

Sikufanikiwa kuchukua ma picha kwasababu nilikua busy sana kabisa, lakini nashukuru sana katika safari zangu zote, Mungu alinirinda sana. Nawatakia siku kuu Njema wadau wangu wote, pia nina Imani katika mwaka wa 2014, unaenda kua mwaka wamafanikio, na katika kazi zangu naenda kujiandaa niwaletee mambo mema kabisa ya kuburudisha ninyi wadau wangu. Tuombeane na Mungu atubaliki kwa pamoja.

Sunday, December 22, 2013

Chiza Joseph kaja na Short Film "HAPPINESS"

Chiza Joseph ni Kijana Mrundi ambapo anaishi Dallas, TX. Kijana huu kaamua kuja na Short Film ambao inaitwa "HAPPINESS" Directed by Young PDK. Nimekubali kazi hii kua wakiendelea ivi, mbele mambo yatakua sawa katika tasnia yetu ya filamu nchini Burundi ao kwa taifa la Warundi. 

Bonyeza Link hii ukatazame nawewe! 
http://www.youtube.com/watch?v=NnjPTcbQoK0&feature=youtu.be

Saturday, August 3, 2013

Deborah Movie Trailer [Burundian Movies]by Aline Vyuka www.burundiango...







Movie Trailer ya filamu tulio shoot. Kueni hewani filamu inakaribia kuondolewa mda si mlefu

Safari yangu kwenda South Dakota katika kazi za ku shoot filamu na Album ya Aline Vyuka

Huyu ni Aline D. Vyuka, msichina anaye kuja na mvuto mkali sana katika nyimbo za Injili, Juzi Juzi nilikua katika mji, wa Sioux Falls, South Dakota anako ishi na tulikua katika shuguri za ku record videos za album yake. Pia tuli shoot movie, ilikua kazi sio mchezo; nilikua uko week mzima na siku 3. Apo kwenye pica alikua akiimba, nami nilikua busy na camera. 

Apa napo alikua alikua akimaliza scene furani, basi akaona akapige mapozi mbali mbali 

Hawa ni wasichana walio msadia kucheza katika nyimbo za alubamu yake, "kuanzia kushoto ni "Mapendo, Jerardine, Merida, Anna" 

 
Basi apo ilikua Sunday baada ya ibada kanisani tukaendelea na shooting. Kabla baada ya kumaliza kazi tunachukua mapozi kido, mbele ni "Jerardine", nyuma kuanzia kushoto ni Diana (naye pia alikua mmoja wapo wa wachezaji katiak nyimbo za Aline Vyuka) wakufuata (in black suit) mwenye The superlative Kaburungu 

Videos niko nazifanyia kazi mambo yatakua noma. kueni hewani, wadau siku zote na endeleeni kunitembelea katika blog yangu

Mana Ndagushima By Aline Vyuka [Official Video] www.burundiangospel.com

Moja wapo wa nyimbo za album yake, basi akapenda ku share na madau, edited by mwenye the Superlative kaburungu. nitakua nawatarifu kazi zangu kama vile nilivyo waaidi wadau wangu, nashukuru kwa ushirikiano wenu na support munao nipa

Wednesday, June 26, 2013

Hassan Assadunllah mmoja wa Burundian Movie Star Nchini Burundi

Kwenye uwanja wa Facebook nimefanikiwa kuongea na Kijana "Hassan Assadunllah" ajulikinae kwa jina la "MUGISHA", huu ni mmoja wa wasanii Nchini Burundi katika tasnia ya filamu.  Filamu aliyo icheza iitwae "MUGISHA" ilio sababisha kijana huu kujulikana Nchini na Nchi za inje, katika maongezi naye kijana huu alisema kua kwa sasa amecheza filamu 6; 3 kwa kirundi, 2 kwa kirafansa, 1 kwa kiswahili. 

Mugisha anasema kua bado yuko katika maendeleo ya filamu. 

Basi ndugu wadau tasnia ya filamu Nchini iko inasonga mbele kama mnavyo ona, nitaendelea kuwapa story hadhisi endapo mukiendelea kuitembelea blog hii. 

NIikajikuta kua napenda blog hii sana

Kwanza natangulia msamaha mkubwa sana kwa ndugu na wadau wote ambapo muko katika maeneo na mikowa mbalimbali. Nime wa miss sana. Katika kwenda kwangu, liniwaambia yakwamba nina blog mpya ambao ilikua www.kaburungu2013.blogspot.com ambapo ilikua kuwaakilisha kazi zangu za mwaka huu wa 2013, ila nimejikuta kua napenda sana blog hii. basi ndugu wadau nimerudia rasmi na twendelee na kazi. 

Kama wengi munavyo kua munafuatia kazi zangu kutumia viwanja vijine vya website, kweli kazi naendelea kama kawaida, na kampuni yangu  Afro Shemeza Stduios" imefanikisha kutengeneza video ya Methuselah mwezi wa pili mwaka huu wa 2013 (Febuary, 2013) 

Thursday, January 24, 2013

Endelea kusoma habari zangu kwa blog mpya

Nimetengeneza blog mpya itakao waakirisha habari za kazi zangu za mwaka wa 2013. Sitakua napatikana katika blog hii kwa kitu kipya, ila ukitaka kusoma habari za zamani, unaweza ukatembelea apa apa, maana itabaki ivi ivi, ila tembelea blog mpya kwa habari mpya kuhusu kazi niko nafanya mwaka huu wa 2013.
www.kaburungu2013.blogspot.com