Monday, March 12, 2012

Bukuru Celestin Amekuja na 1st Album ''Urugendo''


Huu ni Kijana ''Bukuru Celestin'' ambae ni muimbaji wa nyimbo za Injiri. mwaka huu wa 2012 amekuja na album yake ya kwanza inaendakwa jina ''Urugendo'' CDs. katika album hiyo kuna nyimbo kwa luga tofauti zikiwemo Kirundi na Kiswahili. 

Basi ndugu wadau Kijana akapenda ni mtengenezee cover na akapenda kutumia kampuni yangu kwa Duplication. Sauti zimekodiwa katika kampuni tofauti uko anako ishi Roanoke, VA. Ila cover na duplication copies By Seth V. Arts (Afro Shemeza Studios in Association with Victory Studios -www.victorystudios.com).

Natoa shukrani kubwa kwa Kijana huu ambae amemukaribisha Mungu katika maisha yake ili aweze mtumia kwa vipaji mbalimbali alivyo mpa. Ninatoa shukrani pia kwake kwa kueza kuaniamini ili atumie uwezo wangu wakumsaidia katika album yake ya kwanza. kama mnavyo jua, kila kava yote itakao andikiwa ''Seth V. Arts, Afro Shemeza Studios'' mwenyewe The Superlative Kaburungu nimetengeneza. Unaweza kusoma mengi kwa kubonyeza kwenye page ya ''Service'' Ila kwa kazi nyingi mtakua mnaona ''CAG Entertainment, or CAG Pro''

Album imesha ondolewa pateni nakala zenu harisi (original) na si fake. Tujenge uchumi wa Nchi na tuiendeshe kazi ya Mungu mbele.

Monday, March 5, 2012

Johnson Mkubwa pamjona na Radio Rema Fm Burundi Cinema!


Ndugu zangu na wadauu, kijana wangu Johnson Mkubwa apa akiwa anaongea na Mtangazaji wa Radio Rema FM Burundi Cinema Nchini Burundi. 

Jamani ndoto ya Kijana imesha timia. Nimefurahi sana kwa sababu nilikua napenda nihakikishe ndoto yake kama vile vilivyo kuwa nasema na kabisa ametimiza ndoto yake! Ivi sasa Kijana anajulikana kwa Jina "Johnson Mkubwa The Super Star'' Nchini Burundi kwote Kijana huu wanamujua kama J. Mkubwa The Super Star, na kama mlivyo sikia ndani ya maongezi, amesema kua anatarajia pia kwenda Nchini Burundi kucheza filamu na wasanii wa burundi. 

Basi ndugu wa dau maendeleo ni haya, na kama unataka kwendesha mbele kazi yako, mwenyewe the Superlative Kaburungu naweka wote kua wa Super Actors and Stars. Tusaidiane kwendesha kazi mbele na tuendesha Nchi yetu kwa maendeleo kali! Johnson Mkubwa anakuja kwa hali ya juu kuiendesha mbele Nchi yetu Burundi kwa tasnia ya filamu! 

Na Mshukuru Mungu kwa kunipa vipaji mbali mbali na kuweza kuwasaidia wengine wakatimize ndoto zao. Natena Namshukuru Mungu amemuezesha J. Mkubwa kwakufikisha ndoto yake na namtakia kila la heri Mungu amuwezeshe pia kwa mengine zaidi ambae anatarajia kufanya! 

Hongela J. Mkubwa The Super Star

Wednesday, February 29, 2012

Tafadhari ndugu wadau tuwe tunaelewana!

Wadau, kuna mdau ali post comment kwenye wimbo wangu ''Uruwo Gushimwa'' kwenye Youtube akisema hivi, hii ndo comment yake: 
''Nawe vyarakugoyepe! mara Urimumamovie,Mara Mumiziki, Mara muvyimana.
Dufatiki Tureke Iki? ndabaza.Uragahungarema rero ntakundi twabisigura.
Njia mbili zili mshinda mzee fyisi.basi kwarukubazagusa.murakoze kutugezahi.Deney U S A.'' 

Jamani nimefananishwa na Popo! kwa kiswahili uwo jama amesema kua mala nasikika kwenye nyimbo za mungu, mala katika ma filamu, pengine kwa wasanii, eti je ni upande gani nilipo ao niko kama popo? 

Jibu:  Ndugu, jamaa, na mashabiki kama unawazo kama hilo, nataka tuelewe kua kila kipaji kina faida yake. Sijui huu mdau aliona nyimbo nime imba pamoja na mdau wangu Remejio ambae anaishi Seattle, WA; ile wimbo haikukua lengo langu kuiimba! Remejio ni mmoja wa wadau wangu uko Seattle; huu naye ni mmoja kwa walio nipa nguvu kwa kuendelea kazi zangu na kufika mahali nilipo leo. August, 2011 alipenda niimbe wimbo pamoja naye wa kumbukumbu maana nilikua najiandaa kuhamia Hawaii. Ndipo akapenda tuimbe wimbo kuhusu wasichana na akataka nimfanyie video ya wimbo huo. Apo sikukua tayari na vyombo vyangu ili ni mu shoot vyema, ila nikatumia simu tu na jama akashukuru sana kwa hilo. 

Nakama ni Rap kama wimbo ''N'umparire'' ''Oh Dunia'' Jamani Injili ya Mungu haina limit kwa style. Watu wengi hasa warundi, wanajifanya kua niwa kristo sana tena kisana. Nataka tujue yakwamba kila kipaji chochote kile kina faida yake. na kama ni filamu, tujue kua filamu ni moja ya ushauri tena unao badilisha wengi kutokana na ushauri uliyomo ndani ya filamu hiyo. filamu si mbaya, mwanadamu ndo mbaya. kama kuna usherati ndayi ya filamu, haimufanyi ule alio icheza kua msherati, bali ni mashauri wanatoa ya kwamba usherati ni dhambi. Basi kama alio cheza sanaa hiyo ni msherati, hiyo haitasababisha pia kua hiyo filamu ni dhambi ao walio cheza ndani ya filamu kua wote ni washerati. hilo tuelewane. Mimi ni mhubiri tena mtumishi wa Mungu. Neno la bwana linasema hivi: ujihadhae usijifanye kama wewe ni mtakatifu wa sana.'' apo mwenzangu utakua umepotea. Wote tuna tenda dhambi, isipokua tu ukiungama dhambi zako, Yesu ataziosha. 

Tukumbuke mfalme Dawidi kabla ya kubalikiwa kua mfalme, alikua mchunga kondoo. Kipaji chake  alikua akigombana na simba na vingine kama ivyo; ulipo fika wakati goliati akawadhihaki wana Israel eti nani wa kusimama agombane naye? Watu wazima kabisa wakashindwa hata kumsogelea tena walikua na vifaa vya vita ila walishindwa kumsogelea. Kijana mdogo ''Dawidi'' kwa kipaji chake cha kulipua manati, aliweza kumuua Goliati! Jamani vita si vya mwanadamu ni vya Mungu, na kipaji ni balaka za Mungu! kila kipaji kina faida yake. Nami nitatumia kila kipaji Mungu amenipa kwa kumpa heshima zake, ikiwa kuhubiri, nyimbo kwa Rap and Injiri style, filamu, video shooting, editory, design, na mengineo, mimi nitaieneza Injili ya Bwana. Na kama unaona si vyema navyo fanya, basi nikuombe usi nihukumu usije ukahukumiwa mwenyewe. Maana hata na wewe huyajui uyatendalo! kikubwa niombee na nikuombee ila tusi tusane ao tuhukumiane! Tusome neno la Mungu na Tuelewe. 

Asanteni 

The Superlative Kaburungu ''Seth Vyamungu'' 


Friday, February 24, 2012

Kazi ya Mungu Imesonga Mbele

Ndugu wadau, nafikiri siku chache tu nilikua naongelea kua kazi ya Mungu naendeleza pia Mungu anazidi kutuwezesha. Kama nanyi munavyo ona kwenye Head Picture apo Juu, mambo ni hayo. 


Mungu ameweza kubaliki Ministry yetu ya Vijana ivi sasa tuna websites kama www.cagministry.com na ingine ambao inakuburudisha ndani ya Yesu www.cagvoice.webs.com 


Wadau wengi hua wanauliza eti kama nimebadilisha kutokutengeneza filamu tena, jibu ni kwamba apana sijabadilika ila kuigiza nitaigiza katika movie imbao inashikiriana na mambo ya Mungu. Na kama ni ku hariri ama ku shoot filamu iyo naiendelea kama kawa, pia nimefanya mabadiliko kidogo kwamba UGLEAWOOD Entertainment nimeamua kuyiacha na kuanzisha CAG Voice Entertainment. Iyo ndo itakua inawaburudisha ndani ya Yesu na itakua ina protect CDs and DVDs za waimbaji ama wachezaji wa Injili Movies. 


Kazi yangu bado naendelea vile vile ila sitakua na uwezo mkubwa wa kuigiza isipokua tu ni filamu ya Injili. kwa ku edit (uhariri) nitumika kama kawaida, kazi naifanya. ukitembelea apo juu kidogo kwenye ''Services'' page, utaona kazi za utengenezaji nimewai kufanya. 


Kwa kifupu, nawakaribisha nyiye wote kwenye Ministry hiyo tena mukatembelee website zetu na mka waalike wenzenu tukajiunge wote ndani ya Yesu Christo Bwana. www.cagministry.com  or www.cagvoice.webs.com 

Tuesday, January 17, 2012



Basi ndugu wadau mzigo mwenyewe ni huu, nimesha kwisha kuwatengenezea Cover ya movie hii. si mchezo kama nilivyo waambia kua movie hii itakua next level (hatua mbele) kwani hata uonekano wake mwenyewe unatisha. tusubilini nini mwana dada huu (Sarah Lily) ambae ni kizazi kipya katika tasnia yetu ya filamu, nini atakionesha. wadau wengi hua wanauliza je atazidishia Irene Kasongo AKA ''Joanne'' In 21Days? Jibu sina wala Kijana wangu Johnson Mkubwa hana. Jibu ni kwamba siwezi msifia kabla mzigo hujawafikia kwani, ninyi ndo mnapendekeza yupi kafumua mbomba. Hata kijana huu namtakia kufanya zaidi katika mzigo huu.



siku chache nitawapa Trailer ya movie hii, endeleeni na kutembelea blog yangu na tena muishirikishe kwa ndugu na jamaa ili kazi iendelee mbele! ninyi ndo tumaini letu!


Wednesday, January 4, 2012

Kijana anaipeleka UGleawood Movies hapa malekani na Canada, Next level

Ndungu wadau kijana ''Johnson Mukubwa'' anakuja kwa hauta mbele! Muigizaji maarufu ambae anamuonekano wa kutikisa tasnia ya filamu hapa malekani na Canada ambae ni Johnson Mkubwa, nimeamua sasa kuhakikisha anatimiza ndoto yake.

Filamu ''Get Blessed to be Saved'' ni Next Level ya filamu hapa USA na Canada na zingine filamu mbali mbali za ki Africa. Huyu kijana kwa uonekano wake anapenda kuiendesha kazi nzuri sana ya filamu kuenyesha maendeleo zaidi nchini kwetu Burundi. Naye anaonekana ni muigiza maarufu nchini Burundi kwani anaterekeza kuifumua tasnia ya filamu hapa USA-CANADA (Burundian Movies) 

Filamu hii kama nilivyo sema ni Next level yani hatua mbele, nimehakikisha kila kitu kua kamili. Ndani ya movie mutapata mambo mapya ya kuwahakikishia kua movie hii ni Next Level,  yenyewe ni haya:

Best Quality  (Uonekano mkali wa hari ya Juu)\
Best Acting   (Uigizaji wa hari ya Juu)
Best Vision and Editory (Uhariri wa hari ya Juu)
Best Promotion   (Uandaji wa hari ya Juu)
Best Actors   (Waigizaji wa uonekano wa kutisha)

Mwenyewe The Superlative Kaburungu nimehakikisha hayo yote yanapatikana katika movie hii kama munavyo ona hata kwenye pica tu ya usambazaji kua bado inakalibia, wenyewe mnaona hari si kama ya zamani. Mwaka huu wa 2012 ni Mambo mbele, maendeleo kali! kwani kijana huu nimeamua kumuteuwa ili ndoto yake itimie. Mutafikiri kua nami Je nimecheza? Jibu sina ila nawahakikishia kua mimi hasasa na Promote hii filamu, si filamu tu hata kijana huu anapenda sana kuitumia kampuni yangu "Afro Shemeza Studios'' kutokana na kua ndio yenyewe ili muanzisha safari yake ya uigizaji kuanzia ''21Days". Basi kwakifupi ametoa shukurani sana kuona na Muunga mkono na kumusaidia bega kwa bega, hata nami namshukuru kwakuniamini kama naweza chukua hatua hiyo yakumusadia kunyesha uwezo wake.

Chakula Chenu mwaka huu, filamu inakaribia mda si mlefu! endelea kutembelea blog yangu siku chache utaona bonge la Surprise ya kava (cover) ya movie hii,....

Tuesday, December 27, 2011

Kazi naendelea na maendeleo zaidi

kwa kifupi ndugu wadau ni kwamba kweli muda kitambo sipatikani kwenye blog hii ila nikwasababub nilikua nimepatwa namajukumu furani na mengi hivi ya kuwaletea habari njema.


Ndugu wadau ni kwamba mimi wengi nasikia kua wananijua kama Director na nikweli mimi ni Director wala sitabadilika kamwe ila bado naendelea zaidi ya zaidi. Ivi sasa mtakua munanipata kwenye movie za ki Kristo kutangaza injili ya Mungu zaidi kutumia kuhubiri na mambo yama filamu kama munavyo jua wengi kua filamu ni moja kali ya ushauri. Mwaka huu wa 2012 nakuja kiupya tena zaidi ya zaidi kama vile Mungu alivyo agiza na ametimiza. Basi ndugu wadau tuendeshe kazi ya Mungu mbele kwa kukumbuka tulipo anguka na tumurudilie bwana. unaweza kufikiri kua nimeokolea kwa sasa, sikusema ivo ila nikwamba tangu mwanzoni nilikua mkristo ila nilikua na kimbia sana na maisha ya dunia angalau nipate maendeleo ila nigunduwa ni wapi mafanikio anapatikana, ni kwa Mungu kabisa na kwa hivi naendelea sana kwa bidii...


Mwaka wa 2012, Kijana wangu ''Johnson Mkubwa'' anakuja na filamu inaitwa ''Get saved to be Blessed'' chakula ni chenu nitawaeleza ni lini itaondolea maana movie hiyo itafanyiwa kazi (uhariri) na kampuni yangu (Afro Shemeza Studios/Store). kuweni hewani na kutembelea sana blog yangu bila kusahau kampuni yangu ingine ambao inatangaza filamu hizo ''Ugleawood Entertainment''(ugleaworld.ning.com)


Kwa zaidi mwaka huu wa 2012, mutakua munanisikia sana kwa mahubiri ya Mungu na kwa kifupi tuna mkutano wa Vijana July 7-8, 2012 in Dallas, TX  unakaribishwa ndungu mdau kwa kupata balaka kutoka kwa Mungu maana Mungu ameyaanda mengi kwa watu wake! Mengi zaidi mutayajua kwa kufuatia blog yangu na nitapenda sana maoni yenu kwa ku comments hasasa kwenye Ugleaworld.ning.com ili tuendeze kazi mbele!


Karibuni kwa ''The Superlative Kaburungu'' kizazi kipya na ''Maendeleo kali''