Monday, October 22, 2012

Muimbaji wa Nyimbo za Injili "Bukuru Celestin" Kuendelesha mziki wa Yesu Mbele

Picture Taken from Concert during the perfomance


Muimbaji maarufu katika tasnia ya Burundian Gospel Music apa USA "Bukuru Celestin, katika maongezi yangu na yeye Kijana (C. Bukuru), ananieleza yakwamba katika jiji (City) anako ishi Roanoke, VA hua wanafanya ma show na ma Concert, Kijana naye ameipata fursa kubwa sana ya kushiriki katika Concerts hizo. Kama munavyo ona kwenye picha, hapo walikua wakiimba katika moja ya hizo Concert zinazofanyika katika jiji la Roanoke. 

Kijana "Bukuru Celestin" anayo ndoto ya kufanya Band kubwa ambapo atakuwa anafanya utendaji pamoja na Band yake. Kwa maongezi yake, aliniambia yakwamba hata sasa Band amesha ianzisha ivi sasa wapo wanao msaidia kuimba ijapokua anatafuta wapiga vinanda, guitar na ufundi wingi tofauti katika swala la mziki. Katika Band hiyo amewashirikisha dada zake; Furaha, Elvanie, na dada mwingine anaitwa Abia na Kijana mwingine ambae alikua CAG Voice Entertainment Journalist "Jonathan Nyandwi", pia pengine hua anatumia wadada zake wengine kama "Toyi Zawadi, Furaha Chantal" Na hawo ndo alikuja nao katika Mkutano wa CAG Ministry ulio fanyika Jiji la Dallas, Texas mwaka huu wa 2012 mwezi wa 7 tarehe 7 na 8. Kijana alifanya utendaji (performance) mkubwa katika mkutano huo, na katika utendaji huo alimushirikisha tena "Olive Ndayisenga"  ambae ni member wa CAG Ministry kutoka Houston, TX.  Pia Kijana C. Bukuru alikua amekuja na CDs za Album yake ya kwanza "Urugendo"; wengi walifurahia mkanda huo kwa ujumbe uliomwo. 

Ukienda kwenye Facebook yake "Bukuru Celestin" unaweza kuona picha nyingi mbalimbali akiwa anafanya utendaji katika Concerts hizo! Kibinafsi namshukuru sana Kijana huu kwa kweza kumupa nafasi Mungu ali aweze kuindelesha Injili ya Yesu mbele, na katika performances anazo zifanya, yanipa matumaini yakwamba taifa letu la Warundi siku sijazo tutapata maendeleo. Nikweli vijapi tunavyo lakini tunakosa fursa, na pengine sijui yakwamba tunangoja fursa zitutafute ao sisi kuzitafuta! 

Katika Picha kuanzia kushoto ni: Bukuru Celestin, Elvanie, Abia, Furaha, Jonathan Nyandwi. katika mtimbo munawaona wenyewe wazungu wakiwa wanafanya makamuzi katika nyimbo za kiafrika, tena kijana anasema kama katika ma Concerts mengi wazungu wanamusingizia ili waweze kucheza nyimbo zake, naye hana kabisa kipingamizi, Injili ya yesu inaendelea. Nampa Hongela sana Kijana Bukuru Celestin. 

Kama bado hujapata CD yake "URUGENDO" jipatie nakala yako Original kwa sasa

The Superlative Kaburungu

No comments:

Post a Comment