Mapito unayo pitia ndugu yangu ni mda
Ndugu zangu wapendwa, na wasalimu katika Jina la Yesu. Wadau wangu wote na washiliki wa blog yangu hii, leo ningependa tukumbushane machache kuhusu neno la Mungu, safari turio nayo ni ndefu sana, tena tukumbuke ya kwamba safari haikosi makwazo.
Kitabu cha Jeremiah (YEREMIA) 29:11 panasema: "Maana ninajua mawazo niyowawazia, asema BWANA, ni mawazo ya Amani, wala si ya mabaya; kuwapa ninyi Tumaini siku zenu za mwisho (kwa bibilia ya kingereza siku za mwisho ni: Future "siku sizajo mbele"). Hata kama unapitia hayo, ikiwa ni shida, magonjwa, mateso, majaribu, mikosi, nuksi, etc, Ujue kwamba Mungu anakuwazia mema. Hayo yalio kupata si lengo la Mungu, ndo maana anakuandalia mpango mzuri wa kukutoa katika mapito hayo. Bwana yesu alisema katika kitabu cha YOHANA 14:1-3 "Msifadhaike miyoyoni mwenu, mumwamini Mungu muniamini na Mimi. Nyumbani kwa Baba kuna makao (mazuri) mengi, kama hazingekuwepo ninge waambia, tena naenda kuwaandalia pa kwenu. Kwa maana naenda kuwaandalia pa kwenu, nitakuja kuachukua, ili nilipo na nyi muwepo."Alipo Yesu hakuna Shida, magonjwa, matatizo wala majaribu, etc. ila kuna furaha na Amani tele. Basi alipo Yesu lazima na wewe uwepo, ndo ahadi yake njema alio agana nasi. Tukumbuke nabii Musa, Mfalme Farao alifanya amri ya kuuwa watoto wakiume ila Bwana akapanga mpango wa kumuokowa. Mpango wa Farao (hesabu kama Shetani ao aduwi) hukumufikia Musa. Kuna mpango wa Mungu wa kukuokoa ambao bado hujafichua, subiri kwa Imani utaona Mijuiza. Hatuwezi kujua mawazo wala mpango wa Mungu, ila tunalo tumaini katika maandiko yale ya YEREMIA 29:11. Mawazo yake kwako ni ya Amani; ni kwamba anakuwazia mema na anakutakia Amani katika shida zako. Tukifikiria kuhusu hari ya hewa, kuna Summer, Spring na Fall; mda wa fall hua kuna balidi kubwa sana na kuna Nchi ambazo zinafikiwa na balidi kali kabisa hadi mtu kufikiri ahame. Lakini huwezi kutosha matumaini kwasababu ya balidi hiyo, maana Summer ikifika utafurahi hakutokua balidi tena. Basi, usiruhusu mapito yakukoseshe raha ambazo zinakuja mbele yako kama vile Bwana alivyo sema. Simama imara, Mungu atakupigania. Ikiwa ni kwenye ndoa yako, hayo ni mapito tu, tia Imani yako na matumaini yako kwa Yesu Kristo, siku moja utapa amani na mmeo ao mkeo pia na na watoto wako. Mawazo ya Bwana si kama yamwanadamu na Njia zake si kama za mwanadamu, basi kama tunatambua hilo, lipi ambalo Mungu wetu asilo liweza? Bwana anasema yakwamba mwenye haki hatoachwa, bali humulinda na kumukinga na kumuokowa katika shida zake zote. Tafadhari mapito hayo yasikusababishe wewe kumwacha Yesu, songa mbele! Muombe Mungu akufunze kuziendea njia zake zote na kufuata amri zake, maana kuna faida kulijua neno! Mungu wetu anaitwa Mfariji wa Ajabu. Ebu tusikie Bwana alio yasema katika kitabu ya Isaya 41:9-13 "Wewe niliye kushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe Umutumishi wangu; nimekuchaguwa wala sikukutupa. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe; usifadhaike kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama wote waliona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakua si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakua kama kitu kisichokuwa, wale walio fanya vita juu yako. Kwa maana mimi, BWANA, mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume , nitakwambia; Usiogope, mimi nitakusaidia."
Jikaze uyashinde mapito, baada ya hayo utafurahi na hutoyaona tena, Bwana ni mwaminifu kwa wenye haki! Huko peke yako katika shida hizo, Mungu yupamoja nawe! Endelea kwa maombi na Kumusifu Mungu kama vile Paulo na Sila gerezani waliendelea kumsifu Mungu ingawa walikua katika shida. Paulo alisema pia katika kitabu ya WARUMI 8:18 "Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu." Ndo maana nimesema Fall inaweza kukuumiza lakini ukifikia Summer hutokumbuka balidi (mateso) tena. Vumilia upate ushindi maana upo! Yesu alisha maliza kutuonyesha ushindi huo kwa kazi kubwa alio ifanya pale gorigota!
AMANI YA MUNGU IWE NANYI!
The Superlative Kaburungu "Seth Vyamungu"
No comments:
Post a Comment