Sunday, September 30, 2012

Uncle Jimmy Kaleta fursa ya kutisha katika tasnia ya Comedy & Drama

"Uncle Jimmy"
Wadau wangu wote, na Imani huu kijana wengi munamjua katika movie nilio mshirikisha ya 21Days. Kwawalio nunua full original DVD ya movie hii (21days), mwishoni mumeshuhudia Comedy nilio ifanya naye kwa maongezi furani; na ndani ya movie alikuwemo maana alicheza na warembo katika scene ya Club. 

Kijana huu anaenda kwa jina la "Uncle Jimmy"Anaishi Boston, Massachussetts USA.  Katika safari (ao Experience) yakuigiza filamu, kijana huu ametangulia kwa filamu nilio mshirikisha ya 21Days ilio rikodiwa State ya Vermont. Kwa maongezi nilio kua naye, kweli nimejua yakwamba Comedy na Drama anaziweza pasipo masiara. ivi sasa baada ya hayo, amekuja na filamu ya Comedy ambae inaitwa "Crazy family" Na katika kuongea na kaka yake "Felix", nikwamba apo Boston, MA kuna kikosi kali kinatengeza ma filamu; karibu firamu tatu wamesha tengeneza ila bado hazijaondelewa kutokana na kuwaandalia uhariri wa hari ya Juu kwamba watowe mzigo ulio bora. Na katika ma filamu haya mtakutana na Uncle Jimmy kuaburudisha Comedy na Drama zisizo kifani. 

Ebu mwenyewe Jionee Trailer ya "Crazy Family". Bonyeza apa 
Na kwenye Youtube Channel yake inaenda kwajina "Nyandwi Augistine" utashuhudia video zingine zake maana hata maongezi yake mwenyewe yatakuhakikishia yakwamba, burudani ya Comedy ipo kwake. Nakusii madau zangu, malafiki na fans ya blog ao kazi zangu, musikose nakala zengu ndembo za rangi ya kumelemeta yani "Original DVD" mujipatie Burudani. 

Sikiliza alivyo fanya ndani ya 21Days Movie. utamuona kuanzia 2:13 


Kama bado hujapata nakalo yako harisi, ni mda wako sasa wakuipata, wasiliana nasi kwa mengi zaidi. 

Saturday, September 8, 2012

Aline Vyuka AKA "Vyuka" Moja Burundian Artist in the USA

Aline Vyuka AKA Vyuka “Movie Director, Editor, Actress, and Gospel Artist” Msichana huu anatesa BAHOWOOD Entertainment State ya South Dakota, pia ni Kiongozi “Funder and Director” wa BAHOWOOD, Sioux Fall, SD.


Msichana huu naimani wengi munamujua katika movie ariyo igiza “Familly Issues” wengi hapa malekani walipenda movie hityo kwasababu kuna mafundisho mengi ndani ya filamu hiyo. Vyuka pia ni Muimbaji wa nyimbo za Injili (Burundian gospel Artist” kama huja pata bahati ya kusikiriza nyimbo kutoka katika album yake ya kwanza, ni bahati yako sasa.

Sikia wimbo wake, moja kati ya Album yake "VYUKUSENGE"  


Album Trailer:


Hii nazo ni trailer ya movie ariyo tengeneza na kuigiza

Zebedayo "AKA Robert" kafunga Ndoa


Nyawadwi Zebedayo AKA Robert “Actor in 21Days” Kijana kafanya ndoa mwezi wa nane mwaka huu (August, 2012), ameuaga ujana wake ivi sasa ni Mme alio kamilika.


Muigizaji huu hatujui kama ataendelea mambo yake ya movie maana wengi hua wanasimamisha kutokana na mambo ya kifamilia, maana, labda naweza kuendelea ikiwa ni ndoto yake ya kua Staa wa filamu! Mengi zaidi nitawataarifu nikipata habari
Kwenye harusi mambo yakiendelea
Kaburungu pamoja na Zebedayo, ilikua mwezi watatu, mwaka wa 2011 (Boston, MA) katika maandalizi ya 21Days.

Friday, September 7, 2012

Young PDK pamoja na The Superlative Kaburungu kwenye Mkutano

Hawa ni Seth Vyamungu AKA Kaburungu Vs Pierre Lutaka AKA Young PDK katika Mkutano wa CAG Ministry ulio fanyika Dallas, TX July 7-8, 2012. Apa ilikua sunday baada ya mkutano nikiwa na muaga Young PDK na kumushukuru katika ukalimu wake ili aje tukasaidiane katika mambo furani.

Alinisaidia sana katika Mkutano huo maana alikua Camera man kwasababu nilikua na shuguli nyingi kama Msimamizi wa Mkutano huo ilibidi sasa ni kachemshe mambo. Young PDK akishirikiana na mdogo wake "Willy" ndo wa shoot Mkutano huo (Conference), na Video ikaribia kutoka soon, ili muone Jinshi mambo yalikua.

Celestin Niyongabo ambae ni The SYUB Show Camera man, naye alikua akishiriki katika mkutano huo. apo alikua akinionesha mapozi mbali mbali kwamba katika igizo ya Comedy anaweza. Kabisa na mimi nilikubali hadi nikacheza kuzidi kiasi. Kijana huu kwa Comedy, kama una filamu unataka kuizigiza na unaitaji Full original Comedy, na kusihi umupe na fasi kijana huu maana anaweza.

Thursday, September 6, 2012

Pierre Lukata AKA Young PDK

Picture taken in interview with The SYUB Show

Kijana wenye Heshima zake Pierre Lukata ambae anajulikana kwa Jina la “Young PDK” Kijana huu amefanya zake za kuinua Industry ya warundi apa malekani na Inchi mbalimbali za Nje. Pia ni Pruducer wa SYUB Show akishirikiana na Steven Raphael wakitesa apo Houston, Texas.


Young PDK ni Founder and Chair man wa EASTAFRICANHIT.com website hiyo inatangaza habari mbalimbali za wasanii wa warundi na watanzania. Young PDK ni mrundi ambae amezaliwa nchi ya Congo. Katika SYUB Show aliaidi ya kwamba hata waimbaji wa Nyimbo za Njili anawapa karibu awatangazie kazi zao katika website yake. Tembelea website EASTAFRICAN.com utapata kujua mengi kuhusu yeye.

Akiendelea na pozi mbalimbali baada ya Show, nafikiri alikua ana check jinsi Interview ilikua.

Warundi, tusaidiane katika kazi zetu ili tuyiendeshe mbele Nchi yetu ya Burundi. Naimani kuna mabadiliko yanaenda kutokea kwetu sisi warundi hapa malekani tukishirikiana kwa upendo na umoja!

The SYUB Show

MH. (Mheshimiwa) Steven Raphael, nisinge muita kijana maana ana famalia ndo maana nikamuita Mheshimiwa, kwasababu napenda kuwaita ivo walio jenga familia zao.


Steven Raphael ameanzisha Show inaitwa SYUB Show (Sauti Ya Uwamusho Burundi) show hii inakutaarifu kazi za warundi zinazo fanyika apa USA. Show hii inapatikana katika mtandao wa YouTube, ni mda wako sasa wakusikiliza. Tafadhari warundi tusipuuzie maana hii ni moja wapo wakuiendelesha mbele kazi na taifa ya warundi Nchini malekani. Ni waajibu wako sasa wakujua habari tofauti za warundi hapa USA na Nchi zinginezo za Nje.

Kama una Business unataka kutangaza, na unapenda ijulikane watu wakuelewe wewe ni nani, unafanya kazi gani, una mpango upi wa kuinua taifa la warundi, karibu uwasiriane na Steven Raphael kwenye facebook utampata na mtaongeya mengi.

SYUB Show ipo tayari kuinua Burundian Industry apa malekani, karibu uwatembelee kwenye YouTube “The SYUB Show”. The SYUB Show inapatikana Houston, Tx. Kwa mengi zaidi nitawajulisha endapo munaendelea kunitembelea katika blog yangu hii. 


Hii ni Crew (group) ya SYUB Show, kulia ni Willy "SYUB Camera man", katikati ni Steven Raphael "SYUB Representative and Director", kushoto ni Pierre Lukata AKA Young PDK "SYUB Producer and Editor" kuna mwingine ambae haonekani katika picha hii, Celestin Niyongabo "SYUB Camera man.