Tuesday, December 24, 2013

Safari yangu ya kwaga mwaka huu wa 2013, ambapo nilikua Missouri na Colorado

Kwenye picture ni mimi (Right), na Murishi Yaya AKA Solo Kibangu (Left), Kijana huu tumekutania Kansas City Missouri, na kweli nimekubali kazi yake yakupiga guitar cha Solo. Kijana huu tulikua tunaongea kawaida kwenye simu basi ikabidi tuonane uso kwa uso, na baada ya kukutana tukagundua kumbe sisi ni familia kabisa ya ndani.

Kabla kuingia Kansas City, Missouri; nilikua Columbia, Missouri ambapo nilipakaa wiki tatu mzima. Uko nilikua katika kazi ya kutengeneza miziki (Beats) na kweli kama kawaida yangu kwa uwezo wake roho mtakatifu niliweza kuwatengenezea beats zaidi ya 40. Ninavyo vipaji vyingi sana ndani yangu na nimemuaidi Mungu kua nitavitumia vyote kwa pamoja, na nikweli Mungu yupamoja nami katika kazi zote zile.

Sikia wimbo ambao nimefunya na Kijana Murishi Yaya in Kansas City, MO
http://www.youtube.com/watch?v=ubbugPmh7Oc&feature=youtube_gdata

Wimbo haukufanyiwa Mixing kwasababu nilikua katika harakati ya kwenda Denver, Colorado

Baada ya hapo Tarehe 8 mwezi wa December 2013, nikaingia Denver, Colorado ambapo na penyewe nilikua natengeneza Beats za Kwaya furani hivi.

Sikufanikiwa kuchukua ma picha kwasababu nilikua busy sana kabisa, lakini nashukuru sana katika safari zangu zote, Mungu alinirinda sana. Nawatakia siku kuu Njema wadau wangu wote, pia nina Imani katika mwaka wa 2014, unaenda kua mwaka wamafanikio, na katika kazi zangu naenda kujiandaa niwaletee mambo mema kabisa ya kuburudisha ninyi wadau wangu. Tuombeane na Mungu atubaliki kwa pamoja.

Sunday, December 22, 2013

Chiza Joseph kaja na Short Film "HAPPINESS"

Chiza Joseph ni Kijana Mrundi ambapo anaishi Dallas, TX. Kijana huu kaamua kuja na Short Film ambao inaitwa "HAPPINESS" Directed by Young PDK. Nimekubali kazi hii kua wakiendelea ivi, mbele mambo yatakua sawa katika tasnia yetu ya filamu nchini Burundi ao kwa taifa la Warundi. 

Bonyeza Link hii ukatazame nawewe! 
http://www.youtube.com/watch?v=NnjPTcbQoK0&feature=youtu.be